Home BUSINESS MKURUGENZI WA SHEAR ILLUSIONS AHAMASISHA WAZALISHAJI WA BIDHAA ZA NDANI KUZINGATIA UBORA

MKURUGENZI WA SHEAR ILLUSIONS AHAMASISHA WAZALISHAJI WA BIDHAA ZA NDANI KUZINGATIA UBORA

Mmiliki wa kiwanda Cha Zanzibar Handmade Cosmestics Shekha Nasser akizungumza katika mkutano maalum uliokuwa ukijadili masuala mbalimbali zikiwemo changamoto zinazowakabili wanawake na vijana katika Biashara ulioandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la UN-Women wakati wa Kongamano la Wanawake na Vijana lililofanyika kwa siku tatu chini ya Sekretarieti ya AfCTA.

DAR ES SALAAM.

Wazalishaji wa bidhaa za ndani nchini wameshauriwa kuendelea kutengeneza bidhaa zenye ubora zitakazoendana na Soko la Kimataifa ili waweze kujipatia wateja wengi Nje ya nchi.

Hayo yameelezwa jijini Dar es salaam na Mmiliki wa kiwanda cha Zanzibar Handmade Cosmestics Shekha Nasser wakati akifanya mahojiano na waandishi wa habari kuhusu kikao cha wanawake wajasiriamali chenye lengo la kujadili namna ya kuwawezesha kutumia fursa zilizopo Nje ya nchi.

Amesema ni vyema wafanyabiashara wakatumia fursa kujifunza Mafunzo mbalimbali Ili wajiongezee uelewa mkubwa kwani yatawasaidia kutengeneza bidhaa zilizobora jambo ambalo litawawezesha kunufaika na bidhaa zao.

Shekha Nasser amesema kuwa changamoto wanazozipata ni kutokana na baadhi ya wafanyabiashara wengi wa ndani kupenda kutumia bidhaa zinazotoka Nje ya nchi.

“Changamoto nyingine tunazokumbana nazo sisi wanawake wafanyabiashara ni Jinsi ya kupeleka bidhaa Nje ya nchi Kwa mfano kutuma bidhaa Botswana ilihali ipo Afrika”amesema Shekha.

Amesema kama Mhe RAIS amepitisha sheria ya kuwa na Public Procurement Act inayoruhusu kwamba Asilimia 30 ya tenda zote zinazozalishwa serikalini zipewe makampuni yanayomilikwa na wanawake ni vyema hiyo sheria pia ikajaribu kufanya kazi katika Taasisi Binafsi.

Aidha amesema kwa sasa wamejiandaa kuandaa bidhaa Bora ili waweze kufika katika ushindani wa kimataifa Huku akiwaomba TBS kutoa Mafunzo ya mara Kwa mara kwa wajasiriamali Ili waweze kutengeneza bidhaa zenye viwango.

Previous articleMKURUGENZI TPDC AWATAKA WATANZANIA KUCHANGAMKIA FURSA ZA MRADI WA BOMBA LA MAFUTA
Next articleKONGAMANO LA BIASHARA LA WANAWAKE NA VIJANA LA AfCFTA LAFANA JIJINI DAR
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here