Wanufaika wa Mpango wa TASAF wakipewa elimu (warsha za jamii) kabla ya kupokea ruzuku.
Wanufaika Wa Mpango wa TASAF Wakipokea Mafunzo katika Warsha Kabla ya kupokea Ruzuku zao.
Wanufaika Wa Mpango wa TASAF Wakipokea Ruzuku zao
Na: Mwihava GF-Serengeti.
Wanufaika wa TASAF Wilayani Serengeti wameipongeza Serikali kwa kuanzisha mfumo Mpya wa Malipo kwa njia ya Mtandao,ambapo wanufaika wanapokea ruzuku zao kwa kupitia mitandao mbalimbali ya simu ambazo wamejisajili kupitia namba za NIDA. Mfumo huu umesaidia kuongeza usalama wa pesa,pamoja na utunzaji/uwekaji wa akiba kwa wanufaika wanaopokea Ruzuku hizo.
Akizungumza na wanufaika wa Mpango wa TASAF wilayani Serengeti wakati wa zoezi la uhawilishaji fedha,Mratibu wa TASAF Wilayani Serengeti Bi.Antussa William amewasisitiza wanufaika wa Ruzuku hizo kuendelea kuhakikisha wanatumia Ruzuku hizo kama njia ya kujikomboa wao wenyewe kiuchumi,na kuhakikisha wanawekeza katika miradi yenye tija kulingana na mazingira yao.
Aidha,kuhakikisha watoto wao wanaenda shule na vituo vya afya ili waweze kupata ruzuku hizo za masharti. Pia aliwasisitiza walengwa wote kuwahi kwenye vituo vya malipo ili kushiriki kikamilifu warsha za jamii ambazo zinawajengea uwezo wa kuibua na kuinua vipato vyao.
Nao wanufaika wa TASAF wameendelea kuishukuru serikali kwa kuongeza ubunifu katika kuhakikisha kaya zao masikini zinaweza kujisamamia zenyewe kwa kuboresha na kuongeza mifumo mipya.
‘’Kuchukua kwa mtandao mimi naona ni afadhali,kuliko njia ya zamani kwa sababu hii njia hupati usumbufu,na inafanya kutumia Ruzuku hiyo kwa malengo’’alisema Bw.Alex chacha
Lakini pia Walengwa wametakiwa pia kujitokeza kwa wingi wanapohitajika ili kuweza kupata maelekezo mbalimbali kutoka kwa viongozi.