Home Uncategorized KINANA AHITIMISHA ZIARA KWA KUZUNGUMZA NA WANA CCM MKOA WA MWANZA

KINANA AHITIMISHA ZIARA KWA KUZUNGUMZA NA WANA CCM MKOA WA MWANZA

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana, Akizungumza na Viongozi wa Chama, Serikali pamoja na Wanachama wa CCM  wakati wa kuhitimisha ziara yake mkoani Mwanza  kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.  (Picha na Fahadi Siraji CCM Makao Makuu).
MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana, amehitimisha ziara yake mkoani Mwanza kwa kuzunguzumza na wanachama wa Chama hicho kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini humo.
Mkutano huo ulihudhiriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka ambaye amekuwa na Kinana kwenye mikoa yote aliyofanya ziara.
Viongozi wengine waliohudhuria mkutano huo ni  Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mwanza, Anthony Dialo, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Angelina Mabula, wabunge, wajumbe wa NEC,,Mku wa Mkoa wa Mwanza Adam Malima pamoja na  wanachama wengine wa Chama hicho.
Akizungumza na Wana CCM hao Kinana amewahimiza kuendelea kudumisha umoja na mshikamano huku akikumbusha kuwa kwa sasa Chama kipo kwenye mchakato wa kuchagua viongozi hivyo ni vema wakachagua viongozi wenye sifa za uongozi badala ya kuchagua kwa kuangalia urafiki, ukabila au ukanda.
Katika ziara hiyo Kinana ametembelea mikoa ya Kigoma, Kagera, Geita na Mwanza ambapo pamoja na mambo mengine amekutana amekagua miradi ya maendeleo ukiwa utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2020-2025.
Previous articleWAZIRI UMMY MWALIMU ATETA NA MTENDAJI MKUU WA GLOBAL FUND
Next articleDERBY YA DAR ES SALAAM, AZAM NA YANGA HAKUNA MBABE
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here