Home LOCAL KINANA ATEMA CHECHE KAGERA,ATAKA WAKULIMA KUONDOLEWA VIKWAZO

KINANA ATEMA CHECHE KAGERA,ATAKA WAKULIMA KUONDOLEWA VIKWAZO

 

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi wa Wilaya ya Muleba ambao walijitokeza kwa ajili ya kumlaki baada ya kuwasili eneo hilo leo Septemba 2.2022 kuendelea na ziara  ya kikazi mkoani Kagera.

Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania bara Ndugu Abdulrahman Kinana ametoa wito wa kuondolewa kwa vikwazo dhidi ya wakulima pale wanapotaka kuuza mazao yao.

Akizungumza na wana CCM na wananchi waliyojitokeza kumlaki Nyakanazi, Wilaya ya Biharamulo mkoani Kagera, Kinana amesema nia ya mkulima na mfanyakazi ni kuondokana na umasikini na siyo kukutana kubaki katika umaskini kwa sababu ya vikwazo.

“Watu wanalima, watu wanafanyakazi ili kuondokana na umasikini sio kuendelea na umaskini kwa sababu ya vikwazo. Wakati wa kulima hatuwasaidii, wakati wa kupalilia hutuwasaidii, wakati wa kuweka dawa hatuwasaidii,wanapokwenda kuvuna hatuwasaidii, wakishavuna wanataka kuuza wanapoona watapata bei nzuri ndipo na sisi wenye utaratibu tunajitokeza sio sawa.

Ajabu shamba ni la mkulima, kahawa ni yake, mkulima ndio kavuja jasho lakini mnanizuia kuuza ninapoona bei ni nzuri basi nileteeni mwenye bei nzuri niwauzie. Naomba tujiepushe kuwawekea wananchi wetu mazingira magumu wanapotaka kuuza mazao yao.“ alisema Kinana huku akishangiliwa.

Kinana amemuomba mkuu wa mkoa wa Kagera kuwalinda wakulima wanapotaka kuuza kahawa yao nje.

“Hakuna kahawa ya magendo, Kahawa ni yangu nikitaka kuiuza popote kwa yoyote mwenye bei nzuri inakuaje magendo?” Aliuliza Kinana.

Kinana ameongozana na Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Itikadi na Uenezi Ndugu Shaka Hamdu Shaka katika ziara yake iliyoanzia mkoani Kigoma anatarajiwa kuelekea mkoani Geita kabla ya kuhitimisha katika mkoa wa Mwanza

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here