Home SPORTS KIDUKU, MANDONGA WAISIMAMISHA MTWARA

KIDUKU, MANDONGA WAISIMAMISHA MTWARA

 Na:Mwandishi Wetu, Mtwara

MABONDIA Twaha Kiduku na Karim Mandonga jana asubuhi alisimamisha shughuli za kiuchumi kwa muda kutokana na kupewa mapokezi mazito chini ya mkuu wa mkoa, Kanali Ahmed Abasi Ahmed kuelekea kwenye pambano la kimataifa la Mtwara Ubabe Ubabe 2 linalotarajia kupigwa Septemba 24, mwaka huu kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona uliopo mjini hapa.

Katika mapokezi hayo ambayo yaliongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Dustan Kyobya ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya mkoa kutokea katika uwanja wa ndege wa Mtwara kwa kuzunguka mitaa mbalimbali ya mkoani hapa kabla ya kwenda kwa mkuu wa mkoa, Kanali Ahmed Abasi Ahmed ambaye aliwakaribisha mabondia hao mkoani hapa.

Kanali Ahmed alisema kuwa anawakaribisha mabondia hao mashuhuri nchini ndani ya mkoa huo pamoja na kuwatakia ushindi katika pambano lao l la Mtwara Ubabe Ubabe 2 huku akitoa wito kwa wadau kujitokeza kuweza kwenye mkoa huo kupitia sekta ya utalii kutokana na vivutio walivyokuwa navyo.

“Nadhani nisiwe mzungumzaji sana lakini kubwa nawakaribisha Mtwara pamoja na kuwatakia ushindi katika pambano la Mtwara Ubabe Ubabe 2, nichukue tena fursa hii kuwaomba wadau na kuwapongeza wote walioshiriki katika jambo hili kwa kuutangaza mkoa wa Mtwara na huu ndiyo wakati wa wawekezaji kuja kuweza kwenye mambo mbalimbali yakiwemo ya utalii kwa sababu tuna vivutio vingi hapa,” alisema Kanali Ahmed.

Kwa upande wa Kiduku na Mandonga wameshukuru kwa mapokezi hayo makubwa pamoja na kamati yote ya maandalizi ambapo kila mmoja ameahidi kutoa zawadi ya ushindi siku ya Jumamosi kwa kuhakikisha anashinda pambano lake.

Ikumbukwe Kiduku atapanda ulingoni kutetea mkanda wake wa UBO dhidi ya Abdo Khaled kutoka Misri wakati Karim Mandonga akitarajia kupanda ulingoni dhidi ya Salim Abeid kutoka Tanga.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here