Home SPORTS KIDUKU, KHALED KUONESHANA UBABE KESHO

KIDUKU, KHALED KUONESHANA UBABE KESHO

Na: Mwandishi Wetu, Mtwara

BONDIA Twaha Kiduku na na mpinzani wake Abdo Khaled raia wa Misri leo wamepima uzito Kwa ajili ya kesho kupanda ulingoni kuwania mkanda wa UBO Intercontinental katika Mtwara Ubabe Ubabe linalotarajia kupigwa kwenye Uwanja wa Nangwanda wa Sijaona mkoani hapa.

Kiduku na Khaled wa wamepima uzito leo na tayari kwa pambano hilo la uzani wa Super Middle ambalo litachezwa kwa raundi 10 huku wa kazi wa mkoani hapa wakitarajia kushuhudia kutoka kw mabondia hao.

Licha ya kuwepo kwa mapambano ya utangulizi ila bondia Karim Mandonga amekuwa gumzo kubwa kwa watu wa mjini hapa kutokana na umaarufu wa bondia huyo kutoka Morogoro kufuatia mikwara anayowapiga mabondia wenzake licha ya kupokea vichapo mara kwa mara.

Kiduku amewahakikishia watanzania kuwa yupo tayari kuwapa burudani ya ushindi kwenye pambano hilo wakati mpinzani wake akisema kuwa atamaliza raundi kumi za pambano hilo kwa kuamini atamchapa mpinzani wake.

Mbali ya Kiduku, bondia Karim Mandonga ‘Mtu Kazi’ aliyepewa ubalozi wa mkoa wa hapa, ameendelea kuonyesha umaarufu wake kuliko wanasumbwi wengine waliombatana. Mandoga  atacheza na Salim Abeid pambano la raundi nne, Adam Lazaro atatwangana na Francis Miyeyusho, Emiliano Polino atacheza na Osama Arabi.

Selemani Galile atapambana na Shaban Ndaro pambano la raundi sita, uzito wa kati, Nasra Msami dhidi ya Halima Bandola ikiwa ndiyo pambano pekee la wanawake likiwa la raundi sita. 

Alto Kyenga atapambana na Ibrahim Tamba raundi sita, Malik Deo atacheza dhidi ya Bosco Bakari pambano la raundi nne, Paschal Manyota atazichapa dhidi ya Joseph Mchapeni.Mapambano mengine ni Shafii Mohamed dhidi ya Ramadhan Sunya, Iddi Pazi atacheza na Sebaatian Temba, Ayoub Mwankina dhidi ya Shaban Rajabu, Yassin Mbegu dhidi ya Hassan Mgaya. Azizi Salumu dhidi ya Biemo Max.

Previous articleSERIKALI INAENDELEA NA UJENZI WA BOMBA LA MAFUTA GHAFI-MAJALIWA
Next articleDC BAGAMOYO APIGA MARUFUKU WANAFUNZI KUCHEZWA NGOMA ZA UNYAGO
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here