Home LOCAL KATEKISTA MBARONI TUHUMA ZA UBAKAJI MTOTO WA MIAKA 8 GEITA.

KATEKISTA MBARONI TUHUMA ZA UBAKAJI MTOTO WA MIAKA 8 GEITA.

Na. Costantine James, Geita.

Mtu mmoja aliefahamika kwa jina la Athanas Augustino Rugambwa (62) Mkazi wa Mganza wilayani chato Mkoani Geita anashikiliwa na jeshi la Polisi Mkoa wa Geita kwa tuhuma za kumbaka Mtoto wa miaka 8 Mwanafunzi wa darasa la tatu shule ya Msingi Katema.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa jeshi la polisi Mkoa wa Geita Kamishina Msaidizi Henry Mwaibambe amesema mtuhumiwa wa tukio hilo Athanas Augustino Rugambwa (62) ni Katekista na Mkazi wa Mganza.

Mwaibambe amesema Mtuhumiwa huyo mpaka sasa amekamatwa na Jeshi hilo kwa mahojiano na atafikishwa mahakamani pindi upelelezi utakapokamilika amesema mtuhumiwa alitenda tukio hio kwa mlaghai mtoto huyo kumpatia mafundisho ya dini ya ziada kisha kumbaka.

Katika tukio Jingine Kamanda Mwaibambe amesema Jeshi hilo linamshikilia Mashaka Jeremiah mkazi wa mtaa wa Mkoani Mjini Geita kwa tuhuma za kumuua mkewe aitwaye Amina Idd (34) kwa kumchoma kisu zaidi ya mara nane.

Mashaka anatuhumiwa kutenda tukio hilo Augusti 30, 2022 majira ya saa tano usiku nyumbani kwake katika mtaa wa Mkoani kata ya kalangalala Mjini Geita na mara Baada ya kutenda tukio hilo Mtuhumiwa alikimbia kusikojulikana .

Mwaibambe amesema baada ya tukio hilo jeshi la polisi lilianza msako mkali wa Kumtafuta mtuhumiwa huyo na hatimaye kufanikiwa kumkamata akiwa mkoani Kagera na amekiri kufanya kitendo hicho kwa mkewe kwa sababu ya hasira za mkewe kuuza shamba bila kumpa taarifa.

Aidha Mwanamke mmoja aliyetambulika kwa jina la Asia Kibishe (27) Mkazi wa Kijiji cha Nyarututu kata na tarafa ya Bwanga wilaya ya chato Mkoani Geita amekutwa amejinyonga kwa kutumia kipande cha kanga hadi kufa.

Mwaibambe amesema chanzo cha tukio hilo ni Mgogoro kati yake na mme wake baada ya kutuhumiwa kuiba tsh. 10,000 iliyokuwa chumbani kwao kitendo kilichomkasilisha marehemu na kuamua kuchukua hatua za kujinyonga.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here