Home BUSINESS KAMPUNI YA TIGO, HISENSE ZAZINDUA KAMPENI YA ‘WAKISHUA TWENZETU QATAR NA HISENSE’

KAMPUNI YA TIGO, HISENSE ZAZINDUA KAMPENI YA ‘WAKISHUA TWENZETU QATAR NA HISENSE’

Ofisa Mkuu wa Tigo Pesa Angelica Pesha akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya uzinduzi wa Promosheni ya Wakishua Twenzetu Qatar na Hisense na anayesikiliza ni Balozi wa Kampuni ya Simu za Mkononi ya Tigo Feisal Salum Abdallah ‘Feitoto.

Mchezo wa Klabu ya Yanga na Timu ya Taifa ya Tanzania ‘ Taifa Stars” Feisal Salum maarufu Feitoto akizungumza kwa njia ya video Call na Mlinda mlango wa Klabu ya Simba na Timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ Aishi Salum Manula aliyeko nchini Libya.Manula ni Balozi wa Kampuni ya Tigo ambapo ametumia nafasi hiyo kuwashauri Watanzania kushiriki kikamilifu Promosheni hiyo ili kupata nafasi ya kwenda kushuhudia michuano ya Kombe la Dunia.

DAR ES SALAAM.

KAMPUNI inayoongoza katika kuhakikisha Mtanzania anaishi Maisha ya kidijitali, Tigo Tanzania , leo imetangaza ushirikiana baina ya Tigo Pesa na HISENSE (Mshirika Rasmi wa kombe la Dunia la FIFA) Kuingia katika hatua ya pili ya kampeni yake ya wakishua inayojulikana kama wakishua Twenzetu Qatar na Hisense.

Kampeni hii ambayo itadumu kwa muda wa siku 120 imepamba moto zaidi hivi karibuni kufuatia uzinduzi wa kimkakati wa ushirikiano kati ya Tigo na Boomplay katika uzinduzi wa hatua ya kwanza ya kampeni ya wakishua.

Kupitia kampeni ya wakishua twenzetu Qatar na Hisense, wateja wa tigo watakuwa na nafasi ya kushinda furushi la vifaa vya nyumbani kutoka Hisense , zawadi za papo kwa papo za dakika na SMS kwa wateja wote ambao watanunua kifurushi chochote kupitia Tigo pesa.

“Tanzania ina mapenzi makubwa kwenye mpira wa miguu, ili kuimarisha zaidi juhudi zetu za kuongeza ushirikishwaji wa kifedha nchini, uamuzi wa ushirikiano huu na kampuni ya HISENSE umechangiwa kwa kiasi kikubwa na ufahamu wa uwepo wa wapenzi wa mpira na kuwapa wateja wetu ambao wanafanya miamala kupitia Tigo pesa fursa ya kwenda kutazama mechi kubwa zaidi duniani, pia wateja watapata dakika 50 na SMS 200 watakapo nunua kifurushi cha thamani ya Tshs 500 na kuendelea kupitia Tigo pesa” Amesema Angelica Pesha Afisa mkuu wa Tigo pesa.

Pesha alibainisha ya kwamba Tigo pesa ni mtoaji huduma kamili wa huduma za kifedha na tunaona fahari kuwazawadia wateja nafasi ya kutazama mechi kubwa ya kimataifa ya mchezo wa mpira wa miguu kwasababu ni mchezo mashuhuri zaidi nchini Tanzania. Kupitia aina mbalimbali zilizorahisishwa za mifumo ya huduma za kifedha.

Amesema wateja wana nafasi ya kushinda zawadi babu kubwa zinazoweza kubadilisha maisha, ikiwemo tiketi 50 kwenda kuangalia mechi moja kwa moja nchini Qatar au furushi la vifaa vya nyumbani ikiwemo smart Tv, Sound bar, Jokofu na Microwave kutoka Hisense. “Tunaona fahari kuingia katika ushirikiano na kampuni ya Tigo.

“ Tunatambua kwamba watanzania wanapenda mpira na tunataka kuwapa watu fursa ya kupata furaha ya kipekee maishani mwao.Kombe la dunia ni tukio la kukumbukwa na tunataka Tanzania nzima kushiriki na sisi kufurahia tukio hili la kipekee” Anaeleza Jason Xu Meneja Mauzo wa Hisense.

Miamala ya Tigo pesa ikiwemo kulipia bidhaa na huduma kupitia lipa kwa simu, lipa bill, malipo ya serikali, kutuma pesa, kuweka fedha, kuhamisha fedha kutoka benki, kupokea fedha kutoka mahali popote duniani na nyingine nyingi zitampa nafasi mteja kuingia katika droo ya wiki inayotarajia kupata washindi 80 ambapo 50 kati yao watashinda safari iliyolipiwa ya kwenda Qatar na wengine 30 watapata furushi la vifaa vya nyumbani kutoka Hisense.

Hivyo ili kushinda nafasi hii ya pekee maishani ya kusafiri na zawadi nyingine, tunawahamasisha wateja kufanya miamala mingi kadri wawezavyo kupitia App ya Tigo pesa au piga *150*01#

Kwa upande wakeBalozi wa kampuni hiyo, Kiungo wa Klabu ya Yanga na timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’, Feisal Salum ‘Feitoto’ amesema kampeni hiyo itawaleta mashabiki pamoja kuchangamkia fursa ya kuwenda kushuhudia fainali hizo za mwezi Novemba.

“Kampeni hii imekuja wakati muafaka, watanzania wengi wanafuatilia mpira, wanafuatilia mashindano mbalimbali, sasa mbele yetu kuna fainali za kombe la Dunia, Tigo na Hisense wamekuja kuwasaidia mashabiki wenye bahati wanaotumia huduma ya Tigopesa, ninwakati wa kutumia huduma.zao kuweza kujishindia nafasi hizi,” amesema Feitoto.

Amesema katika kampeni hiyo anashirikiana na Balozi mwingine, golikipa wa Simba na Taifa Stars, Aishi Manual ambaye kwa sasa yupo na timu hiyo nchini Libya.

Mwisho.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here