Home LOCAL KAMPUNI YA GRUMET FUND YAWAKETISHA WASICHANA BUNDA, SERENGETI

KAMPUNI YA GRUMET FUND YAWAKETISHA WASICHANA BUNDA, SERENGETI

Mgeni Rasmi Bi.Rehema koka akigawa Mataulo ya kike kwa wasichana 657 waliofika kwenye kongamano hilo.

Mgeni Rasmi katika kongamano hilo Bi Rehema koka akisema Jambo wakati wa mafunzo hayo

Meneja wa Idara ya Maendeleo ya Jamii kutoka Kampuni ya GRUMET Fund Bi.Frida Mollel akisema Jambo wakati wa Kongamano hilo

Wasichana Kutoka Baadhi ya Shule Wilayani bunda na Serengeti wakifatilia mafunzo kwa Makini kutoka kwa wawezeshaji wakati wa Kongamano hilo wilayani Serengeti

Na: Mwihava, GF -SERENGETI

Kampuni ya Grumet Fund kupitia idara yake ya maendeleo ya jamii imetoa mafunzo kwa wasichana 657 kupitia progam ya  girls Empowerment  session tuko pamoja yaliyolenga  juu ya kujitambua ,kujisimamia na kujilinda dhidi ya vitendo vya ukatili  ikiwemo ukeketaji kwa mtoto wa kike.

Sambamba na ugawaji wa taulo za kike 657 ambazo hutukumikia kwa mwaka mmoja ( reusable pads) kwa wasichana nao.

kwa wasichana hao kutoka shule za sekondari  Hunyari, Sazira na Paul Jones za Wilayani Bunda na shule za Sekondari Robanda na Mugumu za Wilayani Serengeti

Akifungua mafunzo hayo mgeni rasmi Bi.Rehema koka mkuu wa idara ya mifugo  wilaya ya Serengeti amewasihi wasichana kujisimamia na kutokukimbilia mila potofu lakini pia ameishukuru na  kuipongeza kampuni ya Grumet Fund kwa kuweza kujitoa kuwapa elimu wasichani katika mkoa wa Mara ikiwemo Serengeti ,aidha amesisitiza wasichana hao kuhakikisha wanasoma kwa bidii ili kutimiza ndoto zao pamoja na kuwepo kwa vikwazo mbalimbali vinavyowazunguka.

‘’Najua katika kusoma mnapitia changamoto mbalimbali lakini changamoto mojawapo  ni ya Karo ambayo raisi wetu Samia Suluhu Hassani  ameitatua,pamoja na kutatuliwa kwa changamoto hiyo  zipo changamoto za mila potofu zinazomuathiri mtoto wa kike,Hedhi ambayo huwatesa baadhi ya wasichana na kuwapotezea muda kutokana na visumbufu vichache,lakini pia umbali baadhi ya watoto wa kike pamoja na changmaoto ya kukatishwa tamaa’’alisema Bi.Rehema.

Nae,Meneja wa maendeleo  ya jamii kutoka kampuni ya Grumet Fund Bi.Frida mollel amewataka mabinti kujitambua na kujitegemea bila kusubiri watu wengine kuwafanyia maamuzi ya maisha yao haswa katika vitu visivyofaa vinavyoharibu maisha yao ya sasa na baadae.

‘’Sisi Grumet Fund tumekuja hapa kuwapa nguvu na kuwambia kwamba mabinti mnahaki ya elimu,lakini mnahaki ya kusema hapana dhidi ya mila potofu zinazowagandamiza  ikiwemo ndoa za utotoni,ukeketaji,mimba za utotoni mnahaki ya kujisimamia na kuachana na makundi potofu’’alisistiza Bi.Frida

Mtaalamu wa afya kutoka hospitali  teule ya nyerere (NDDH  )Bi.Restuna mluta amewakumbusha wasichana waliohudhuria mafunzo hayo kuwa wanapoonza hedhi ni kiashiria kwamba wako tayari kubeba ujauzito na kuitwa mama,amewataka kuzingatia umri salama wa wao kupata mimba kwani kupata ujauzito katika umri mdogo kunaweza kupelekea madhara kwa mama na mtoto ataezaliwa, aidha amewataka wasichana kujikinga kwa mimba za utoto kwa kusema hapana ,lakini pia kuzingatia masomo  na hatimaye kutimiza ndoto zao.

Kwa upande wa Afisa dawati la jinsia  na watoto wilaya ya Serengeti Bi. Sijali Nyambuche amewafundisha wasichana aina mbalimbali za ukeketaji lakini pia amewakumbusha  kuwa mkoa wa Mara ni miongoni mwa mikoa inayotekeleza vitendo vya ukeketaji  hivyo amewataka wasichana kutokukubali vitendo hivyo kutokana na madhara makubwa yanayojitokeza kutokana na kukeketwa hivyo amewataka wasichana hao kufika katika maeneo salama ili kutofanyiwa vitendo hivyo.

Nao wasichana waliopata mafunzo hayo kupitia kongamano hilo wameishukuru kampuni ya Grumet Fund kwa kuweza kuwapa elimu hiyo na kuiomba serikali na wadau wengine kuongeza Zaidi makongamano ya aina hiyo ili kuweza kuelimika Zaidi.

Mafunzo hayo yamewakutanisha wasichana kutoka katika baadhi ya shule zilipo wilaya ya bunda na Serengeti,ambapo yalifadhiliwa na kampuni ya Grument Fund.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here