Home LOCAL DC SHIMO, VIONGOZI SIMAMIENI ULINZI SHIRIKISHI KATIKA MAENEO YENU.

DC SHIMO, VIONGOZI SIMAMIENI ULINZI SHIRIKISHI KATIKA MAENEO YENU.

Charles Kazungu Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Geita.

Wilson Shimo Mkuu wa Wilaya ya Geita

Luteni Kanali Jelemia S. Mahinya Mshauri wa Jeshi la hakiba wilaya ya Geita.

Charles Kazungu Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Geita.

Na: Costantine James, geita.

Viongozi mbalimbali ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Geita wametakiwa kuimarisha ulinzi shirikishi katika maeneo yao kwa lengo la kukabiliana na changamoto ya matukio ya uporaji pamoja na ujambazi katika maeneo yao.

Rai hiyo imetolewa na Mkuu wa wilaya ya Geita Mhe.Wilson Shimo katika mkutano wa nne wa kawaida wa baraza la Madiwani kwa mwaka wa fedha 2021/2022 uliofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita Nzera kwa lengo la kupokea na kupitisha taarifa za utekelezaji wa shughuli za maendeleo kwa kipindi cha Mwezi Aprili hadi Juni 2022.

Mhe. Shimo amesema ni vyema kuimalisha ulinzi shirikishi katika mbalimbali ndani ya halmashauri ya wilaya ya Geita pamoja na kuwa na vijana wa jeshi la hakiba wenye mafunzo dhabiti ili kusaidia kupunguza matukio ya uporaji pamoja na ujambazi katika maeneo yao.

Kauli hiyo inakuja siku chache baada ya Majambazi kuvamia kituo cha mafuta cha Bageni Katika kijiji cha Ikina kata ya Bukoli wilayani Geita mkoani humo na kumjeruhi kichwani milinzi Obed Stephano katika kituo hichocha mafuta.

Mhe. Shimo amesema katika tukio hilo walibaini walinzi waliokuwepo katika kituo hicho mmoja hakuwa na mafunzo ya jeshi la hakiba hata kidogo hivyo amezitaka kampuni zinazo ajiri walinzi kuajiri vijana wenye mafunzo ya jeshi la hakiba ili waweze kutimiza majuku ya ipasavyo

Mshauri wa jeshi la hakiba wilaya ya Geita Luteni Kanali Jelemia Mahinya amewataka madiwani pamoja na viongozi mbalimbali wa halmashauri hiyo kuwaruhusu vijana kujiunga na mafunzo ya jeshi la hakiba.

Amesema vijana wakipatiwa mafunzo ya jeshi la hakiba itawasaidia vijana hao kujpatia fursa mbalimbali kama vile usimamizi katika mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta hivyo wakipata mafunzo itawaandaa kuzichangamkia fursa.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita Mhe.
Charles Kazungu amesema swala la ulinzi na usalama ni jambo la kuzingatiwa na amewataka madiwani kusimamia vyema swala la ulinzi na usalama katika maeneo yao.

Mhe. Kazungu amewashauri madiwani wa halmashauri hiyo kukaa na wafanyabira pamoja na wadau mbalimbali wa maendeleo katika kata zao kwa wale ambao hawajenga vituo cha polisi kushirikiana na wadau hao ili kujenga vituo vya polisi kwa lengo la kupunguza uhalifu katika maeneo yao.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here