Home LOCAL DC BAGAMOYO APIGA MARUFUKU WANAFUNZI KUCHEZWA NGOMA ZA UNYAGO

DC BAGAMOYO APIGA MARUFUKU WANAFUNZI KUCHEZWA NGOMA ZA UNYAGO

Mkuu wa Wilaya ya BAGAMOYO Zainab Abdallah (katikati)akizindua kitabu Cha mwongozo wa Elimu Msingi na Elimu Sekondari Wilayani BAGAMOYO Septemba 22/2022 (kushoto )Afisa Elimu wa Halmashauri ya BAGAMOYO Wema Kajigile na Afisa Elimu Sekondari Alois Kaziyareli (Na Heri Shaaban BAGAMOYO)

Mkuu wa Wilaya ya BAGAMOYO Zainab Abdallah (katikati)akizindua kitabu Cha mwongozo wa Elimu Msingi na Elimu Sekondari Wilayani BAGAMOYO Septemba 22/2022 (kushoto )Afisa Elimu wa Halmashauri ya BAGAMOYO Wema Kajigile na Afisa Elimu Sekondari Alois Kaziyareli (Na Heri Shaaban BAGAMOYO)

Na: Heri Shaaban (Bagamoyo)

Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Zainab Abdallah amepiga marufuku Wanafunzi kuchezwa ngoma za unyago mpaka wamalize kidato cha nne .

Mkuu wa Wilaya Bagamoyo Zainab Abdallah, aliyasema hayo katika kikao cha wadau wa sekta ya Elimu Wilayani Bagamoyo kilichoandaliwa na Halmashauri hiyo wakati wa kuzindua mwongozo wa Elimu msingi na sekondari .

“Natoa agizo kuanzia leo MARUFUKU wanafunzi kuchezwa ngoma mpaka wamalize shule kidato cha nne nikisikia Mwanafunzi anachezwa unyago ajafika kidato cha nne Wazazi nitawakamata na kuwachukulia hatua “ alisema Zainab.

Mkuu wa Wilaya Zainab alisema Wazazi wengi wanacheza watoto wao ngoma wakiwa wadogo Elimu ya Msingi hivyo wanapevuka mambo ya kikubwa kabla muda wao kufika inapelekea kuingia vishawishi vya kikubwa na kukatisha masomo kwa mimba za utotoni .

Katika hatua nyingine ameagiza Wanafunzi wa shule za Msingi na Sekondari wapimwe afya kabla kwenda Likizo itasaidia kujua malezi ya shule ya Mwalimu na Wazazi awapo nyumbani wakati wa likizo Ili wasipate mimba .

Wakati huo huo AMEAGIZA shule zote Halmashauri hiyo Wanafunzi wapewe chakula asubuhi na jioni kwa ajili ya kuongeza mikakati ya ufaulu Darasani na kukuza taaluma.

Alisema Mwanafunzi akipata chakula wakati wa masomo akili yake inakuwa sawa na kupelekea kufanya vizuri kitaaluma .

Akizungumzia mikakati yake sekta Elimu BAGAMOYO kujenga chuo cha ufundi VETA na Matawi ya vyuo vikuu Ili Wanafunzi walipo Wilaya BAGAMOYO waweze kupata Elimu .

Mwisho

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here