Mwenyekiti wa CCM kata ya Ilala Habib Nasser akizungumza na Wana CCM Ilala Bungoni Leo Septemba 10/2022
Viongozi wa CCM Ilala wakiwa katika ziara ya chama Ilala Bungoni katika mkutano wa Mwenyekiti wa CCM kata kuwashukuru wanachama wake Leo Septemba 10/2022
Na: Heri Shaban (llala)
CHAMA cha Mapinduzi CCM Kata ya ILALA imewataka Wana CCM wa chama hicho kuvunja makundi ndani ya chama wawe wa moja kujenga chama na SERIKALI .
Hayo yalisemwa na Mwenyekiti wa CCM Kata ya ILALA Habib Nasser, wakati wa ziara yake ya kuwashukuru wanachama wa chama hicho wa Ilala Bungoni pamoja na kuwataka wavunje makundi kushirikiana kufanya kazi za chama na Serikali.
“Chaguzi za chama ngazi ya Kata kwa Sasa zimeisha Naomba wanachama CCM tuvunje makundi ya Uchaguzi tushirikiane kwa pamoja kujenga chama chetu cha mapinduzi na Jumuiya zake tuwe wa Moja kujenga Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kumsaidia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan alisema Nasser .
Mwenyekiti wa CCM Habib aliwataka Wana CCM Ilala kutoa ushirikiano kwa Viongozi wao Kata wakiwemo Wenyeviti wa Serikali za MITAA ,Diwani wa Kata ya Ilala SAADY KIMJI na Mbunge wa Jimbo la Ilala Mussa Zungu .
Alisema maendeleo ya Kata ya Ilala kwa Sasa Ilala itakuwa ya kisasa na Maendeleo yanakuja kwa kasi katika utekelezaji wa Ilani ya chama cha mapinduzi CCM.
Alisema dhamira ya ccm kushika Dora katika chaguzi zake za Serikali za MITAA 2024 na 2025 katika Uchaguzi Mkuu wa Wabunge na Madiwani .
Katika ziara hiyo ya kuwashukuru wanachama anaambatana na Watendaji wa Kata na Wenyeviti wa Serikali za MITAA kwa ajili ya kuchukua kero ambazo zinajitokeza katika ziara hiyo .
Wakati huo huo katika ziara hiyo ilibuka KERO ya Mikopo kwa Wananchi wa Ilala ,
Mwenyekiti wa Serikali za Mtaa Bungoni Ally Mshauri, aliwataka Wana ccm wa Ilala kuunda vikundi vyao vya mkopo kwa kufuata taratibu mpya za Mtandao Ili vikundi vya Ilala viweze kutambulika Halmashauri katika mfumo waweze kukopa mikopo ya Wanawake,Vijana na Watu Wenye Ulemavu ambayo Serikali wameelekeza ngazi ya Halmashauri.
Mwisho