Home LOCAL CAMBRIDGE EDUCATION TANZANIA NA TAMISEMI YAWAJENGEA UWEZO MAAFISA HABARI MOROGORO

CAMBRIDGE EDUCATION TANZANIA NA TAMISEMI YAWAJENGEA UWEZO MAAFISA HABARI MOROGORO

Thadeus Rodney Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari Maelezo anayeshughulikia Habari akiongea na maafisa habari wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya Siku Tatu mkoani Morogoro Septemba 19, 2022 yaliyoandaliwa na Cambridge Education Tanzania.

Washiriki wa Mafunzo wakimsikiliza Mkurugenzi Msaidizi wa Habari Thadeus Rodney wakati wa kufungua mafunzo hayo.

Na: Devotha Changh’a: 

Maafisa habari nchini wameshauriwa kuifahamu miradi ya maendeleo na kuitambulisha kwa jamii kuanzia hatua ya mwanzo, namna itakavyotekelezwa na faida yake kwa wananchi wa wilaya na mikoa waliyomo.

Ushauri huo umetolewa na Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari Maelezo anayeshughulikia Habari, Rodney Thadeus katika ufunguzi wa mafunzo ya Siku tatu kwa maafisa Habari mjini Morogoro.

Mafunzo ya mfulilizo yakuimalisha ujuzi wa maafisa habari yaliyoandaliwa na Cambridge Education Tanzania na TAMSEMI ya kuwajengea uwezo katika kusambaza taarifa za mradi wa elimu bora kwa wanavulana, wasichana na walemavu uitwao “Shule Bora programu” mpango wa miaka 6 unafadhiriwa na shirika la UKaid la Uingereza.

Rodney amewaambia wadau wa habari toka mikoa ya Pwani, Tanga na Dodoma kuwa mafunzo hayo kuhusu mradi wa Shule Bora ni manufaa kwao, hivyo ni vizuri miradi hii inapotekelezwa wananchi wa maeneo husika wakajua Serikali yao pamoja na wadau wa Maendeleo ikiwemo UK aids wanafanya jambo gani kwa nchi.

“Ni jukumu la wanahabari kuhakikisha tunatumia vyombo vya mawasiliano kama radio za kijamii, mitandao ya kijamii ili kuwafikishia taarifa walengwa kulingana na maeneo walipo kwenye mikoa na Halmashauri. Tumieni vikao vya maamuzi vya wakurugenzi kupenyeza taarifa na kueleza mipango yenu,” amesisitiza.

Raymond Kanyambo meneja wa mawasiliano wa shirika la Cambridge Education Tanzania amefafanua kuwa mradi huo utaboresha na kuhuwisha mitaala ili iendane na wakati ikiwemo ya watu wenye ulemavu na kuimarisha mifumo ya ufundishaji. Vilevile mradi wa Shule Bora utawajengea uwezo walimu, na kuhakikisha watoto wote wanaoanza elimu ya awali wanafanikiwa kumaliza elimu ya msingi na kuendelea zaidi.

Innocent Byarugaba kutoka Halmashauri ya Kibaha Mkoa wa Pwani ambako ndiko mradi wa Shule Bora ulizinduliwa mwezi April Mwaka jana, amesema: “Tunaufurahia mradi huu kwa kuwa utakwenda kumaliza changamoto na kero zinazowakabili watoto Shuleni, watapata elimu Bora.”

Mradi huu unatekelezwa kwenye mikoa tisa nchini ikiwemo Kigoma, Tanga, Pwani, Dodoma, Mara, Simiyu, Singida, Katavi na Rukwa. Mradi wa Shule Bora ni wa Serikali unaofadhiriwa na Shirika la Maendeleo la Uingereza (UK aids) kwa gharama ya Euro 89 million sawa na fedha za kitanzania Shilingi Bilioni 271.

Mwisho

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here