Home LOCAL BILIONI MOJA KUTATUA KERO YA MGAO WA MAJI GEITA MJI.

BILIONI MOJA KUTATUA KERO YA MGAO WA MAJI GEITA MJI.

Wilson Shimo Mkuu wa Wilaya ya Geita.

Frank Changawa Mkurugenzi mtendendaji GEUWASA

Mradi wa Chujio la maji Nyankanga.

Keneth Sindro Meneja Uendeshaji wa Kampuni ya Gipco.

Na: Costantine James, Geita.

Serikali kupitia Mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira Mjini Geita (GEUWASA) imetenga kiasi cha bilioni moja kwa ajili ya upanuzi wa chujio la maji katika chanzo cha maji Nyankanga kwa lengo la kutatua changamoto ya utoshelevu wa maji ndani ya Geita mji.

Mkurugenzi mtendaji wa Mamlaka ya maji na usafi wa mazingira mjini Geita mhandisi Frank Changawa amesema wanatekeleza mradi huo wa upanuzi wa chujio la maji katika chanzo cha maji Nyankanga kwa lengo la kuongeza wigo wa upatikanaji wa maji ndani ya Geita mji.

Upanuzi wa chujio la maji katika chanzo cha maji Nyankanga utasaidia kuongeza uzalishaji wa maji kutoka lita milioni 4 hadi kufikia lita mioni 7 kwa siku hivyo kuwezesha kupunguza adha ya ukosefu wa maji safi na salama ndani ya Geita mji.

“kwa sasa hivi wananchi wanaitaji maji kwahiyo tumechukua hatua za dharura kutanua chujio letu la maji kutoka lita milioni 4 hadi lita milioni 7 kwa siku” amesema Mhandisi Frank Changawa .

Meneja ufundi wa Mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira mjini Geita Mhandisi Izack Mgeni amesena eneo la Nyankanga ndipo kilipo chanzo kikuu cha maji kinachohudumia maji mji wa Geita kwa sasa mtambo ulipo katika chanzo hicho unauwezo wa kuzalisha lita laki mbili kwa saa sawa na wasitani wa lita milioni 4 kwa siku.

Mhandisi Izack amesema kwa sasa miundombinu ya kutibu maji katika chanzo hicho inazalisha si zaidi ya asilimia 30% ya mahitaji kwa siku hali inayosababisha kuwepo adha ya mgao wa maji katika maeneo mbalimbali ndani ya Geita mji.

Amesema Geuwasa imeanza utekelezaji wa mradi huo kupitia fedha za serikali kwa kupanua chujio la kuchujia maji kutoka lita laki mbili mpaka lita laki tatu na nusu kwa saa ambapo itawezesha kuongeza hali ya uzalishaji wa maji kutoka lita laki 4 kwa siku hadi lita milioni 7 lengo likiwa kuongeza hali ya upatikanaji wa maji ndani ya Geita mji.

Meneja uendeshaji wa kampuni ya Gipco Keneth Sindiro amesema utekelezaji wa mradi huo umeanza mwezi 4 mwaka huu na unaendelea vizuri mpaka sasa umefikia asilimia 60% unatarajiwa kukamilika ifikapo Novemba 2022.

Mkuu wa wilaya ya Geita Mhe. Wilson Shimo amekili kuwepo na changamoto ya mgao wa maji ndani ya Geita Mji hivyo serikali kupita Mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira (GEUWASA) wameamua kupitia mradi huo kutatua changamoto hiyo ili kuwawezesha wananchi kupata maji safi na salama ya kutosha katika maeneo yao.

Mhe. Shimo amemtaka mkandarasi anaesimamia mradi huo wa upanizi wa chujio la maji kuhakikisha anakamilisha kawakati kama ilivyopangwa ili kuwaondole kero wananchi ya kupata maji kwa mgao.

“Rai yangu kwa mkandarasi kuhakikisha kwamba mara fedha itakapo ingia kama ambavyo tumeahidiwa na serikali yetu pendwa mkandarasi akamilishe kazi hii ndani ya mwezi novemba” Amesema Mhe. Wilson Shimo Mkuu wa wilaya ya Geita.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here