Home LOCAL BALOZI MULAMULA ASHIRIKI MKUTANO WA 12 WA MAWAZIRI MARAFIKI WA UN WA...

BALOZI MULAMULA ASHIRIKI MKUTANO WA 12 WA MAWAZIRI MARAFIKI WA UN WA USULUHISHI

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe Balozi Liberata Mulamula akishiriki Mkutano wa 12 wa Mawaziri Marafiki wa Umoja wa Mataifa wa Usuluhishi unaofanyika sambamba na Mkutano wa 77 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa jijini New York.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe Balozi Liberata Mulamula akijadiliana jambo na washiriki wa Mkutano wa 12 wa Mawaziri Marafiki wa Umoja wa Mataifa wa Usuluhishi uliofanyika jijini New York.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe Balozi Liberata Mulamula akiwa katika Mkutano wa 12 wa Mawaziri Marafiki wa Umoja wa Mataifa wa Usuluhishi ujijini New York.
Wenyeviti wenza wa Mkutano wa 12 wa Mawaziri Marafiki wa Umoja wa Mataifa wa Usuluhishi Uturuki na Finland wakiwasikiliza washiriki wa kikao hicho.
 
 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe Balozi Liberata Mulamula ameshiriki Mkutano wa 12 wa Mawaziri Marafiki wa Umoja wa Mataifa wa Usuluhishi unaofanyika sambamba na Mkutano wa 77 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa jijini New York.
 
Akizungumza katika mkutano huo Balozi Mulamula amesema usuluhishi ni njia muhimu katika kutatua changamoto za migogoro duniani na kuusihi Umoja wa Mataifa kuliingiza suala la usuluhishi katika mifumo ya utatuzi wa migogoro ya Umoja wa Mataifa.
 
Amesema usluhishi ukiingizwa katika mifumo ya utatuzi ya migogoro ya Umoja huo utasaidia shughuli za upatanishi na utatuzio wa migogoro na hivyo kuufanya Umoja huo kufikia lengo la utatuzi wa migogoro na kuifanya dunia kuwa sehemu salama .
Previous articleMANDONGA, KIDUKU WAPEWA UBALOZI WA KUITANGAZA MTWARA
Next articleMAKAMU WA RAIS AHUTUBIA MKUTANO WA GLOBAL FUND
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here