Home INTERNATIONAL UN WOMEN YASISITIZA KUFANYIWA KAZI MAPENDEKEZO YA KONGAMANO LA AfCFTA LILILOFANYIKA JIJINI...

UN WOMEN YASISITIZA KUFANYIWA KAZI MAPENDEKEZO YA KONGAMANO LA AfCFTA LILILOFANYIKA JIJINI DAR

Mwakilishi Mkazi wa UN Women Tanzania Hodan Addou (kushoto) akizungumza alipokuwa akiongoza mkutano wa wanawake kutoka katika nchi mbalimbali Barani Afrika kujadili changamoto zinazowakabili wanawake na vijana katika Biashara na kupokea maoni ya wadau hao namna ya kufanyiakzi changamoto. Kikao hicho kilifanyika Septemba 14,2022 wakati wa kuhitimisha Kongamano la Afrika la Wanawake na Vijana katika Biashara chini ya Sekretarieti ya Eneo Huru la biashara Barani Afrika (AfCFTA) Jijini Dar es Salaam. (katikati) ni Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya jinsia na Wanawake, Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Grace Mwangwa, na (kulia) ni, Mkuu wa Uwezeshaji wa wanawake kiuchumi wa UN Women kutoka New York Marekani Jemima Njuki.

(PICHA ZOTE NA: HUGHES DUGILO)

Na: Hughes Dugilo. DAR ES SALAAM

Kutekelezwa kwa vitendo maadhimio ya kongamano la wanawake na vijana katika biashara  Barani Afrika kutarahisisha kuboresha mazingira bora na wezeshi kwa wanawake na vijana  kufanya biashara zao ndani ya Afrika bila vikwazo.

Ni wazi kwamba wanawake wafanyabishara katika Bara la Afrika wamekuwa wakitamani sana kupata fursa ya kufanya bishara zao kwa uhuru utakaowawezesha kutoka nchi moja hadi nyingine bila vikwazo vyovyote lakini wameshindwa kutokaka na kukosekana kwa  miundombinu rafiki na wezeshi  ya kibiashara.

Kutokana na Changamoto hizo Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya Wanawake la UN Women liliwaketisha wadau kutoka katika nchi mbalimbali za Afrika katika mkutano uliojadili kwa pamoja changamoto za wanawake wa Afrika katika biashara na  namna ya kuzipatia ufumbuzi.

Mkutano huo ulifanyika Septemba 14, 2022 wakati wa kuhitimisha Kongamano la Siku tatu la Wanawake na Vijana lililofanyika kuanzia Sept.12, hadi 14, 2022 Jijini Dar es Salaam chini ya Secretariati ya Eneo huru la Biashara katika Bara la Africa (AFCFTA).

Mkuu wa Uwezeshaji wa wanawake kiuchumi wa UN Women  New York Marekani Jemima Njuki aliipongeza Sekretaeiti ya AFCFTA kwa kushirikiana na wadau wengine wa maendeleo, na Serikali kwa hatua kubwa waliyofikia ya kuwakutanisha wanawake na vijana kutoka mataifa mbalimbali ya Afrika kujadili kwa kina, na kisha kutoka na mapendekezo ya pamoja ili  nchi wanachama wanaotekeleza mkataba wa AFCFTA kuyafanyia kazi kwa mustakabali wa nchi hizo na Afrika kwa ujumla.

Amesema anaamini Serikali za nchi wanachama wa AfCFTA zitakwenda kuyapitia na kuyafanyiakazi mapendekezo yote yaliyotolewa kwenye Kongamano hilo na hatimaye kufikia hatua ya kuondolewa kwa vikwazo vinayowakwamisha wanaawake na vijana katia kufanya bishara.

Ameongeza kuwa wanawake pamoja na vijana  wanakabiliwa na changamoto kubwa ya kupata elimu namna  ya kuweza kuboresha biadhaa zao.

“Wanawake wanatakiwa kupewa elimu ya ubora wa Bidhaa Ili kuweza kutumia vizuri fursa za kiuchumi zinazotolewa Barani Afrika” 

“kutokana na muamko wa utoaji wa elimu kwa wanawake na vijana imesaidia kwa kiasi kikubwa kuweza kuwekeza katika uchumi ili kuweza kufikia asilimia 50 ya Uwezeshwaji wa wanawake na vijana Barani Afrika. ameongeza.

Kwa upande wake Afisa Programu kwa upande wa kuwawezesha wanawake kiuchumi wa Shirika la UN Women Tanzania, Michael Jerry amesema pamoja na mambo mengine Kongamano hilo pia limejadili masuala ya sera zitakazoweza kufungua fursa mbali mbali za masoko katika Eneo huru la Biashara Afrika kwa wanawake na vijana.

“Kongamano hili limewezesha kuwakutanisha wadau mbali mbali kwa lengo la kusikiliza na kuboresha changamoto zinazowakabili vijana na wanawake katika suala zima la uchumi,”amesema Jerry.

Amesema baada ya kusikiliza changamoto hizo ni jukumu lao kwenda kuzifanyia kazi kwa vitendo ili kwenda sambasamba na kasi ya ukuaji wa kiuchumi Afrika.

mwisho.

Mkurugenzi wa Chama cha Wafanyabishara Wanawake Tanzania Mwajuma Hamza akizungumza kwenye mkutano huo.
Mshiriki wa mkutano huo kutoka Afrika ya Kusini Phelisa Nkemo akizungumza alipokuwa akichangia mada kwenye mkutano huo.
Mmiliki wa kiwanda Cha Zanzibar Handmade Cosmestics Shekha Nasser akizungumza katika mkutano huo akitoa mchango wake wa nini kifanyike katika kushughulikia  changamoto zinazowakabili wanawake na vijana katika Biashara ulioandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la UN-Women Jijini Dar.
Dkt. Christine Oyenak kutoka Sudan ni moja ya mdau aliyeshiriki katika mkutano huo akizungumza kuelezea nini kifanyike katika kushughulikia changamoto zilizopo katika nchini za Afrika zinazosababisha kuwepo kwa vikwazo kwa wanawake na vijana kufanya Biashara.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here