Home INTERNATIONAL

Na: Mwandishi wetu, DAR ES SALAAM.

Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini Tanzania Chirstine Musisi amesema kuwa uwepo wa Kongamano la Wanawake na Vijana katika Biashara chini ya Mkataba wa AfCFTA kumeleta hamasa kubwa na kuibua changamoto za kibiashara Barani Afrika.

Musisi ameyasema hayo alipokuwa akitoa hotuba yake katika Kongamano hilo katika hafla ya kufunga rasmi Septemba 14,2022 Jijini Dar es Salaam.

Amesema kuwa Mkutano huo umepata mafanikio makubwa kutokana  na maazimio ya pamoja ya mkutano huo yatakayotoa dira kwa viongozi wa Afrika kuandaa Sera na mipango ambayo itakuwa rafiki kwaajili ya kuboresha na kuinua Biashara za wananchi kwa manufaa ya jamii na Mataifa kwa ujumla.

Amesema wanawake ni nguzo Kuu inayofanyakazi na kwamba anaamini kupitia Sera nzuri na endelevu zitazidi kuwajengea mazingira bora ambayo utekelezaji wake utatoa majibu muhimu kwa mustakabali wa uchumi endelevu katika jamii na Bara la Afrika kwa ujumla.

“UNDP na UN-Women tupo tayari kusaidia na kufanikisha mipango yote ambayo imedhamiria kuinua Biashara zinazoongozwa na wanawake. Hivyo kuwapa dira Ili waweze kushiriki Ili waweze kushiriki kikamilifu katika Biashara” amesema.

Aidha amesema kuwa UNDP na UN-Women wako tayari kufanyakazi na wanawake ikiwemo Secretarieti  AFCFTA Ili yale yote yaliyojadiliwa katika Kongamano hilo yaweze kuingia kwa haraka katika utekelezaji ili kuleta ufanisi kwa manufaa ya wanawake na vijana Barani Afrika.

Kongamano la Wanawake na Vijana katika Biashara Afrika limefanyika kwa siku tatu Jijini Dar es Salaam Tanzania kuanzia Septemba 12 hadi 14, 2022 na kuhudhuriwa na wadau kutoka katika Mataifa mbalimbali ya Afrika kwalengo la kujadili changamoto zinazowakabili wanawake katika Biashara na kuzipatia ufumbuzi

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here