Home SPORTS TAIFA STARS YACHAPWA 3-0 UGENINI UGANDA IKIFUZU CHAN

TAIFA STARS YACHAPWA 3-0 UGENINI UGANDA IKIFUZU CHAN

TANZANIA imetupwa nje ya mbio za kuwania tiketi ya Fainali za Ubingwa wa Mafaifa ya Afrika (CHAN) baada ya kuchapwa 3-0 na Uganda katika mchezo wa marudiano raundi ya mwisho ya mchujo leo Uwanja wa St. Mary’s Kitende mjini Entebbe.

Mabao ya yaliyoizamisha Taifa Stars yamefungwa na Moses Waisa dakika ya 17 kwa penalti, Richard Basangwa dakika ya 52 na Rogers Mato dakika ya 75 na sasa The Cranes wanafuzu Fainali za CHAN zitakazofanyika nchini Algeria kuanzia Januari 8 hadi 31 mwakani.

The Cranes inafuzu kwa ushindi wa jumla wa 4-0 baaa ya kuichapa Taifa Stars 1-0 kwenye mechi ya kwanza Jumapili Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam, kipigo ambacho kilifanya kocha Mdenmark, Kim Poulsen aondolewe na Mzambia, Hanoor Janza kupewa timu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here