Home SPORTS YANGA YAANZA VYEMA LIGI KUU YAICHAPA 2-1 POLISI TANZANIA

YANGA YAANZA VYEMA LIGI KUU YAICHAPA 2-1 POLISI TANZANIA

 

MABINGWA wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania bara timu ya Yanga imeanza vyema katika kutafuta taji la 29 baada ya kutoka nyuma na kushinda mabao 2-1 dhidi ya wenyeji Polisi Tanzania mchezo uliopigwa uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.

Polisi walipata bado dakika ya 34 likifungwa na Salum Kipemba baada ya Bakari Mwamnyeto kufanya makosa lililosababisha kumchanganya Mlinda mlango wake Diarra.

Akitoka kukosa Penalti Mshambuliaji hatari Fiston Mayele aliisawazishia Yanga dakika ya 41 baada ya kutokea piga ni pige kwenye lango la Polisi hadi mapumziko timu zote zilienda zikiwa nguvu sawa.

Kipindi cha pili Timu zote zilifanya mabadiliko na mnamo dakika ya 85 Nahodha Bakari Mwamnyeto  kuipatia Yanga bao la ushindi akimalizia pasi ya Benard dk 85 Pasi Morrison.

Mchezo mwingine umepigwa uwanja wa Liti Mkoani Singida wenyeji Singida Big Stars wamepata ushindi wa bao 1-0 dhidi Tanzania Prisons.

Ligi hiyo itaendelea kesho kwa michezo minnet Coastal Union atacheza na KMC jijini Arusha, Dodoma jiji watacheza na Mbeya City uwanja wa Liti Singida,Simba watakuwa uwanja wake wa Benjamin Mkapa kucheza Geita FC na mchezo wa Mwisho Azam FC watawakaribisha Kagera Sugar.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here