Kaimu SAfisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Vipimo Tanzania (WMA) Bi. Stella Kahwa (mwenye nguo ya kitenge) akiwahudumia wananchi katika maonesho ya Nanenane yanayofanyika katika Viwanja vya John Mwakangale Jijini Mbeya.
Afisa Vipimo wa WMA Edward Hiza akitoa elimu kwa wananchi waliotembelea kwenye Banda la Taasisi hiyo kufahamu namna wanavyotekeleza majukumu yao katika Maonesho ya Nanenane Jijini Mbeya.
Meneja wa WMA Mkoa wa Mbeya Albogasti Kajungu (kulia)a kitoa elimu kwa wananchi katika maonesho hayo.
Na; Hughes Dugilo, MBEYA.
katika kuhakikisha wananchi hususani wafanyabiashara na wakulima wanapata uelewa juu ya matumizi sahihi ya vipimo Wakala wa Vipimo Tanzania (WMA) imetoa elimu kwa wadau na wananchi mbalimbali wanaotembelea katika maonesho ya wakulima nanenane yanayofanyika katika viwanja vya john Mwakangale Jijini Mbeya.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Agosti 6,2022 katika maonesho hayo Meneja wa wakala wa Vipimo (WMA) Mkoa wa Mbeya albogasti kajungu amesema wamekuwa wakitoa elimu kwa wananchi namna bora ya matumizi sahihi ya mizani iliyothibishwa na kuhakikiwa na taasisi hiyo.
Amesema kuwa taasisi hiyo ina jukumu la kusimamia vipimo vilivyopo kwenye vifungashio ili kuhakikisha ujazo ulipo unakuwa sahihi kulingana na aina ya ujazo wa bidhaa husika.
“Wakala wa Vipimo tumeshiriki kwenye maonesho haya kwa lengo la kutoa elimu juu ya matumizi sahihi ya vipimo pamoja na shughuli nyingine tunazozifanya kwa mujibu wa sheria”amesema Kajunngu.
Ameongeza kuwa katika kuhakikisha wafanyabiashara wanafuata sheria na kutumia vipimo sahihi wamekuwa wakifanya ukaguzi wa kushtukiza katika maeneo mbalimbali ya wafanyabiashara ikiwemo mipakani ili kubaini kama kunakuwepo na udanganyifu wowote wa vipimo katika bidhaa zao.