Home LOCAL WAZIRI SIMBACHAWENE: MZEE KUSILA AMEFANYA MAMBO MENGI YA KUIGWA

WAZIRI SIMBACHAWENE: MZEE KUSILA AMEFANYA MAMBO MENGI YA KUIGWA

Mhe. Adamu Kimbisa akisaini Kitabu cha maombolezo nyumbani kwa Mzee William Kusila.

Waziri wa Nchi Ofisi ya waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene akisaini kitabu cha maombolezo nyumbani kwa Mzee William Kusila.

Waziri wa Nchi Ofisi ya waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene akitoa heshima za mwisho wakati wa kuaga Mwili wa Mzee William Kusila katika ibada ya mazishi iliyofanyika nyumbani kwake Kijiji cha Mtitaa-Bahi Mkoani Dodoma.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule akitoa heshima za mwisho  wakati wa kuaga mwili wa Mzee William Kusila.

OFISI YA WAZIRI MKUU.

Na: mwandishi wetu

Waziri wa Nchi Ofisi ya waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene amesema Mzee William Kusila alipenda kuona viongozi wanazingatia miiko, na kuishi kwa kuwa mfano mwema kwa jamii.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene alipokuwa akitoa salamu za serikali katika ibada ya mazishi ya Mzee Williamu Jonathan Kusila aliyezaliwa Mwaka 28/02/1944 na kufariki 21/08/2022,  iliyofanyika nyumba kwake kata ya Mtitaa-Bahi Dodoma 26/August/2022.

“Mzee kusila ni kipimo cha mtu muadilifu; mtu mwenye Upendo, na mtu aliyefanya mambo mengi mazuri ambayo tunapaswa kuyaiga na kuyaenzi.”

Tumepoteza kiongozi wa kisiasa aliyeshika nafasi mbalimbali za umma na kutimiza majukumu yake ipasavyo, ni mtu aliyepinga na kukataa rushwa, alisema Waziri.

Aidha ametoa rai kwa Watoto wa Mzee Kusila kuzidi kushirikiana na kushikamana ili kutunza jina na heshima ya baba.

“Amefafanua watu hawazaliwi sawa, mtatofautiana kwa uwezo wa elimu, uwezo wa kipato na mambo mengine lakini wote ni Watoto wa mzee Kusila ni lazima mtengeneze mamlaka itakayosaidia kuwaongoza kama familia”

Naye  Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule amesema  Mzee William Kusila alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Saba wa Dodoma kati ya Mwaka (1993-19995) alikuwa Mbunge wa jimbo la Bahi na katika vipindi tofauti amekuwa waziri wa kilimo, Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi na amewahi kuwa Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi Mkoa wa Dodoma.

“Alifanya kazi kwa upendo Mkubwa; aliokuwa nao kwa wananchi wa Dodoma, Baba yetu aliongoza kwa Vitendo na sio kwa kuagiza, kama alisema limeni nayeye alikuwa analima”

Naye Mbunge Mstaafu wa jimbo la Chilowa Mhe. Hezekiah Chibulunje akitoa salamu za rambirambi amesema anamkumbuka mzee Kusila kwa jitihada zake za kuondoa Njaa Dodoma na kuhakikisha tunapanda mazao yanayostahimili ukame.

“Alikuwa na uchungu sana katika kuondoa njaa na vile vile katika swala la zima la kusimamia elimu, nimefanya naye kazi kwa ushirikiano mkubwa sana bila nongwa”

Previous articleMIRERANI YATOA BILIONEA MPYA WA TANZANITE
Next articleKUNA MATUMAINI MAPYA TASNIA YA HABARI: NEVILE MEENA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here