Home LOCAL WAZIRI SIMBACHAWENE: KAZI NDIO HESHIMA YA MTU.

WAZIRI SIMBACHAWENE: KAZI NDIO HESHIMA YA MTU.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. George Simbachawene akizungumza wakati wa Sherehe za kumweka wakfu Askofu wa  tatu wa Kanisa  la Anglikana Dayosisi ya Mpwapwa, Rev. George Chiteto iliyofanyika Jijini Dodoma.

Askofu wa  tatu wa Kanisa  la Anglikana Dayosisi ya Mpwapwa Jijini Dodoma. Rev. George Chiteto (aliyelala)  akiwekwa wakfu kuwa Askofu wa kanisa hilo.

Askofu Mkuu wa Kanisa Anglikana Tanzania Mhashamu Dr. Maimbo  Mndolwa akifafanua jambo wakati wa ibada ya kumweka wakfu Askofu wa  tatu wa Kanisa  la Anglikana Dayosisi ya Mpwapwa, Rev. George Chiteto iliyofanyika Jijini Dodoma

Baadhi ya waumini wakifuatilia matukio mbalimbali katika ibada hiyo.

Picha ya pamoja baada ya ibada ya kumweka wakfu Askofu wa  tatu wa Kanisa  la Anglikana Dayosisi ya Mpwapwa, Rev. George Chiteto iliyofanyika Jijini Dodoma.

(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)

Na: Mwandishi wetu- Dodoma

Wakristo nchini wametakiwa kufanya kazi kwa bidii ili kujietea maendeleo, changia pato la Taifa  na kutatua changamoto zilizo katika maeneo yao.

Hayo yameelezwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene wakati akizunguma katika sherehe ya kumweka wakfu Askofu wa  tatu wa Kanisa  la Anglikana Dayosisi ya Mpwapwa, Rev. George Chiteto iliyofanyika Jijini Dodoma baada ya aliyekuwa askofu wa kanisa hilo Askofu Donald Mtetemela kumaliza muda wake .

Waziri Simbachawene alisema chanamoto nyngi za kiuchumi katika jamii zitatauliwa endapo wananchi watajituma kufanya kazi na kuwa wabunifu   kwa kuanzisha miradi mbalimbali kama ambavyo maandiko matakatifu yanaagiza watu kufanya kazi.

“Lazima wakristo wa sasa tufanye kazi lazima tutae changamoto kwenye maeneo yetu maana imeandikwa katika biblia asiyefanya kazi na asile kwahiyo kufanya kazi ndio uhai wako, heshima yako na ukizalisha utaweza kuendesha maisha yako binfasi, utashiriki katika kazi ya Mungu na Taifa zima,” alisema Waziri Simbachawene.

Pia aliongeza kwamba serikalii itaendelea kushirikiana na taasisi za dini kwani zimekuwa na mchango mkubwa katika maendeleo, kusimamia maadili na kupambana na vitendo vya mmomonyoko wa maadili kwa baadhi ya watu wasiyo na hofu ya Mungu.

“Licha ya mchango mkubwa wa kanisa hili kwa serikali lakini kumekuwa na mmomonyoko wa maadili, magonjwa na majanga mbalimbali hivyo ni muhimu kushirikiana na serikali ili kuokoa vijana na watoto wetu na ni matumaini yetu viongozi wa dini mkiendelea kusimama  imara  na kutoa huduma ya kiroho tutatatua changamoto hii,” alieleza.

Aidha alibainisha kwamba Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan imeendelea  kuchukua hatua za kisheria kwa watu wote wanaojihusisha na vitendo vya rushwa , ufisadi, utovu wa nidhamu kwa watumishi wa umma pamoja na jamii kwa ujumla.

Kwa upande wake Askofu Mkuu wa Kanisa Anglikana Tanzania Mhashamu Dr. Maimbo  Mndolwa aliipongeza serikali kwa kuwa mstari wa mbele kuziunga mkono taasisi za dini  katika nyanja zote huku akimtaka Askofu Chiteto kufanya kazi kwa kumtegemea Mungu hatimaye kufikia malengo ya kanisa.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary  Senyamule  alitoa wito kwa wakazi wa mkoa huo kutumia fursa ya serikali  kushusha bei ya  mbolea kwa kujikita katika kilimo.

MWISHO.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here