Home BUSINESS WAZALISHAJI WA BIDHAA MWANZA WATAKIWA KUZINGATIA MISINGI YA USHINDANI

WAZALISHAJI WA BIDHAA MWANZA WATAKIWA KUZINGATIA MISINGI YA USHINDANI

Na: Paul Zahoro Mwanza RS

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe. Adam Malima amewataka wazalishaji na wafanyabiashara mkoani humo kuzingatia misingi ya Ushindani kwa mujibu wa taratibu za nchi ili kulinda mustakabali wa ukuaji wa uchumi wa nchi.

Mhe. Malima ameyasema hayo wakati ajifungua Semina ya uhamasishaji wa masuala ya udhindani na udhibiti wa bidhaa bandia kwa wazalishaji iliyofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza leo, agosti 18, 2022.

“Ushindani una misingi ya kufuata, watanzania tuna mgogoro wa viwango na ushindani tena wa ndani na wa nje lakini lazima tuzingatie ubora wa bidhaa zetuna kusema tu bidhaa ni bidhaa na tukifanya hivyo tutasaidia kukuza uchumi wa nchi yetu.”

Aidha, ameishukuru Tume ya Ushindani kwa mafunzo hayo murua ambayo yatawasaidia wafanyabiashara kufahamu masuala ya udhibiti wa bidhaa bandia na kuwapitisha kwenye sheria na wajibu wa Mtumiaji wa bidhaa na huduma wanazojihusisha nazo.

Vilevile, ametoa wito kwa Tume ya Ushindani nchini kuangalia ubora wa bidhaa nchini kwa kulinganisha na hali ya bei kwenye bidhaa hasa za viwandani na ujenzi ambako ni sekta nyeti kwa maendeleo ya makaazi ya wananchi na ameahidi kushurikiana nao kwenye eneo hilo.

Naye William Erio, Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ushindani (FCC) amesema katika kutekeleza malengo ya serikali ya kuvutia wawekezaji na kuhimarisha uwekezaji nchini taasisi hiyo imeweka kanuni na taratibu za kuhakikisha bidhaa zinazotumika nchini zinakua bora na si bandia na kwamba mlaji na mfanyabiashara haumii kwa namna yoyote.

“Shughuli zenu haziishii kwenye kuzalisha pekee bali bali uingizaji wa biashara hapa nchini sasa sisi tunasimamia ubora wa bidhaa na kuhakikisha wafanyabiashara hawajihusishi na bidhaa bandia hivyo ni lazima mfuate kanuni na taratibu kuhakikisha mnasajiri biashara zenu” Amesema Erio.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here