Home BUSINESS WANANCHI WAMIMINIKA BANDA LA BRELA KUSAJILI BIASHARA ZAO MAONESHO YA NANENANE...

WANANCHI WAMIMINIKA BANDA LA BRELA KUSAJILI BIASHARA ZAO MAONESHO YA NANENANE JIJINI MBEYA

Afisa wa kutoka Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni wa BLERA Anna Nderingo (kushoto) akimkabidhi Cheti mwaandishi wa habari mwandamizi kutoka mkoa wa Mbeya Emmanuel Lengwa (kulia) mara baada ya kukamilisha usajili wa jina la biashara kwa lengo la kutaka kuanzisha TV Mtandao (Online TV) katika Maonesho ya Nanenane yanayoendelea katika viwanja vya John Mwakangale Jijini Mbeya. 

BRELA imeshiriki Maonesho hayo kwa lengo la kutoa elimu kwa wananchi kufahamu shughuli wanazozifanya na kutoa huduma za usajili wa majina ya biashara sambamba na kutoa vyeti papo kwa hapo.

Afisa wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni wa BLERA Anna Nderingo (kushoto) akimkabidhi zawadi ya kikombe mwandishi wa habari Emmanuel Lengwa mara baada ya kusajili jina la Biashara yake na kufanikiwa kupewa Cheti chake Papo kwa hapo.

Mwanasheria wa BRELA Lupakisyo Mwambinga (wa pili aliyekaa) akitoa huduma kwa wateja waliofika kwenye Banda la taasisi hiyo kufanya uhakiki wa taarifa za Kampuni yao katika Maonesho ya Nanenane Jijini Mbeya.

Maofisa wa BRELA wakiendelea na majukumu yao ya kuwahudumia wateja waliofika katika Banda lao kupata huduma. (kulia) ni, Afisa Tehama wa BRELA na (kulia kwake) ni Mhasibu wa Taasisi hiyo Anna Nderingo.

Maofisa wa BRELA wakiendelea kuwahudumia wananchi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here