Home LOCAL UWT MISUNGWI YAKABIDHIWA MIZINGA 50 YA NYUKI

UWT MISUNGWI YAKABIDHIWA MIZINGA 50 YA NYUKI

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Mary Masanja (Mb) amekabidhi mizinga ya nyuki 50 kwa Jumuiya ya Wanawake Tanzania (UWT) ya Wilaya ya Misungwi kwa ajili ya kuendeleza mradi wa ufugaji nyuki.

Akizungumza leo katika Ofisi za UWT Misungwi Mhe. Masanja amesema mizinga hiyo imegharimu kiasi cha shilingi milioni tano.

“Naahidi kuongeza mizinga mingine endapo itaendelea kuleta faida kwa jumuiya” Mhe. Masanja amesisitiza.

Amefafanua kuwa mradi huo wa ufugaji nyuki utasaidia mapato ya jumuiya kutokana na mazao ya nyuki ambayo ni asali, nta, sumu ya nyuki na maziwa ya nyuki mbayo soko lake ni la uhakika.

Mhe. Masanja amefafanua kuwa kupitia mapato yanayotokana na miradi ya jumuiya, itaiwezesha kujisimamia yenyewe hasa katika kukidhi mahitaji muhimu ya wanajumuiya.

Aidha, amewapongeza viongozi wa UWT Misungwi kwa kusimamia vizuri miradi ambapo wameweza kuzalisha lita 40 za nyuki zenye thamani ya shilingi laki nne kutokana na mizinga ya nyuki mitano ya awali.

Pia, Mhe. Masanja ameahidi kuipatia jumuiya hiyo pikipiki nyingine baada ya pikipiki ya kwanza aliyowapatia kukusanya zaidi ya shilingi milioni moja.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here