Home BUSINESS TWCC YAPELEKA WAJASIRIAMALI ZAIDI 100 MAONESHO YA KILIMO NANENANE JIJINI MBEYA

TWCC YAPELEKA WAJASIRIAMALI ZAIDI 100 MAONESHO YA KILIMO NANENANE JIJINI MBEYA

 
Picha za Baadhi ya wajasiriamali katika maonesho hayo.

Tazama Video Hapa

https://youtu.be/RunQZis_cbQ

Na: Hughes dugilo, MBEYA.

Chama cha Wafanyabiashara Wanawake Tanzania TWCC kimeshiriki Maonesho ya Nanenane yanayofanyika Kitaifa katika Viwanja vya John Mwakangale Jijini Mbeya huku wajasiriamali zaidi ya mia moja walipo chini ya TWCC wakishiriki.

Akizungumza katika mahojiano maalum na waandishi wa habari viwanjani hapo Mkurugenzi Mtendaji wa TWCC Mwajuma Hamza amesema kuwa Chama hicho lengo la kushiriki maonesho hayo ni kutoa fursa kwa wajasiriamali wao husani wanaojihusisha na kilimo na usindikaji kukutana na wadau katika sekta hiyo ili kuongeza wigo wa kujifunza zaidi na kupata soko la bidhaa zao.


Amesema kuwa Maonesho ya Mwaka huu ni mazuri sana kwa kuwa kumekuwepo na taasisi nyingi zilizoshiriki maonesho hayo na kwamba hiyo itatoa fursa pana kwa wananchi wanaotembelea maonesho hayo hususani wakazi wa Jiji la Mbeya na mikoa ya jirani kujionea bidhaa mbalimbali zikiwemo za kilimo katika maonesho hayo.


“Nipende kuwapongeza sana waandaaji wa maonesho haya mikoa yote sita ya Nyanda za Juu Kusini wakiwemo wenyeji wa Mkoa huu kwa kuandaa maonesho haya kwa ustadi wa hali ya juu. Haya ni maonesho makubwa sana kuna washiriki wengi sana humu ambapo unaweza kutembelea mabanda uzimalize, haya ni mafanikio makubwa sana” amesema Mwajuma.


Ameongeza kuwa katika maonesho hayo wamekuja na wajasiriamali wanaojihusisha na kilimo pamoja na wanaoongeza thamani katika bidhaa za kilimo wakiwemo wasindikaji pamoja na bidhaa nyingine hivyo kutoa mwito kwa wananchi wanaofika katika maonesho hayo kutembelea Banda lao lililopo eneo la Jukwaa kuu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here