Mtakwimu kutoka Tume ta Madini Tanzania Azihara kashakara (kushoto) akizungumza na wananchi waliojitokeza kaatika Banda la Tume hiyo kujifunza kaazi mbalimbali zinazotekelezwa na Tume hiyo kwenye Maonesho ya Nanenane ynayofanyika Kitaifa katika viwanja vya John mwakangale Jijini Mbeya.
Neema Mwenunge afisa kodi wa Tume ya Madini Tanzania akitoa elimu juu ya aina mbalimbali za madini yanayozalishwa hapa nchini kwa wananchi waliofika katika Banda la Tume hiyo kwenye Maonesho ya Nanenane Jijini Mbeya,
Mjiolojia kutoka Tume ya Madini Hemedi Sarumbo (wa pili kulia) akielezea aina mbalimbali za madini kwa wananchi waliotembelea katika Banda la Tume hiyo kupata elimu juu ya shughuli wanazozzifaanya katika Maonesho ya Nanenane Jijini Mbeya. PICHA: HUGHES DUGILO.
Na: Hughes Dugilo, MBEYA. Tume ya Madini Tanzania imeendelea kutoa elimu kwa wananchi mbalimbali waliotembelea katika Banda la Tume hiyo katika Maonesho ya Nanenane yanayofanyika Kitaifa kwenye Viwanja vya John Mwakangale Jijini Mbeya.
Akizungumza katika maohojiano maalum na waandishi wa habari katika Banda la tume hiyo viwanjani hapo Afisa Madini Wilaya ya Chunya Mhandisi Sabai Nyansiri amesema kuwa lengo la kushiriki kwenye Maonesho hayo ni kutoa fursa kwa wananchi kupata elimu juu ya shughuli mbalimbali zinazofanywa na Tume hiyo pamoja na kujifunza aina tofauti za madini yanayochimbwa hapa nchini.
Amesema kuwa Tume hiyo ina majukumu tofauti katika sekta ya madini ikiwemo kusimamia utoaji wa vibali na kushughulika na upangaji wa bei ya madini pamoja na kudhibiti Mapato yatokanayo na maadini sambamba na kudhibiti utoroshaji wa madini. “Tume ya madini ndio inayoishauri Serikali kuhusiana na masuala yote ya usimamizi wa madini hapa nchini ili mwisho wa siku wananchi wote na Serikali tuweze kufaidika na madini ambayo mungu ametupatia katika nchi yetu“amesema Mhandisi Nyansiri.
Kwa upande wake Afisa Madini Mkazi Mkoa wa Songwe Mhandisi Laurent Mayalla amesema kuwa wapo katika Maonesho hayo kuonesha fursa zilizopo katika sekta ya madini na kuwahimiza wananchi kutembelea katika Banda la Tume hiyo kujifunza na kufahamu fursa hizo. TAZAMA VIDEO HAPA.