Home LOCAL TMDA YAWATAKA WAFANYABIASHARA KUACHA KUUZA DAWA ZA MIFUGO KWENYE MAGULIO

TMDA YAWATAKA WAFANYABIASHARA KUACHA KUUZA DAWA ZA MIFUGO KWENYE MAGULIO

Meneja wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) Kanda ya Nyanda za Juu Kusini,Anitha Mshighati akizungumza na waandishi wa habari katika banda la mamlaka hiyo wakati akielezea kuhusu dawa za mifugo katika Maonesho ya Kilimo-Nane Nane 2022 yanayofanyika Kitaifa kwenye uwanja vya John Mwakangale mkoa wa Mbeya.
 
Meneja wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Anitha Mshighati akitoa maelezo kwa mmoja wa wananchi waliofika katika banda la mamlaka hiyo wa katika Maonesho ya Kilimo-Nane Nane 2022 yanayofanyika Kitaifa kwenye uwanja vya John Mwakangale mkoa wa Mbeya.
Mariam Sanga Afisa Elimu kwa Umma TMDA (kushoto) na  Jofrey Kikoti (kulia) Mkaguzi wa Dawa msaidizi wa TMD wakiwa tayari kutoa elimu kwa wananchi.

Mariam Sanga Afisa Elimu kwa Umma TMDA (kushoto) akimhudumia mwananchi aliyetembelea kwenye banda lao.
 
Na: Hughes Dugilo, MBEYA.
 
Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) imetoa wito kwa wafanyabiashara wanauza Dawa za Mifugo kuacha kuuza Dawa hizo katika magulio na badala yake kufuata utaratibu uliokweka kisheria wa kuwa na maduka maalum ya Dawa hizo.
 
Akizungungmza katika mahojiano na waandishi wa habari katika Maonesho ya Kilimo Nanenane yanayofanyika Kitaifa kwenye uwanja wa John Mwakangale Jijini Mbeya, Meneja wa TMDA Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Anitha Mshigati  amesema kuwa kumekuwepo na tabia ya baadhi ya wafanyabiashara wanaouza Dawa za mifugo kwenye maeneo ya wazi yakiwemo magulio jambo ambalo ni kinyume cha sheria. 
 
“Moja ya jukumu letu ni kusimamia Dawa za Mifugo katika hili tunahakikisha Dawa hizo zinahifadhiwa vizuri kwenye maduka maalum lakini tumekuwa tukipata changamoto kubwa kwa wauzaji wa Dawa hizo kufanya biashara  kwenye magulio jambo ambalo linaweza kuzifanya dawa hizo kuwa hafifu pia ni kinyume cha sheria”
 
“Uuzaji wa Dawa za Mifugo kiholela una madhara makubwa kwa watumiaji kwa kukosa maelekezo sahihi namna ya kuzitumia na kusababisha madhara kwa mifugo inayopelekea vifo au kwa mfugaji kupata hasara kwa kukosa mazao ya mifugo yasiyo kuwa katika kiwango kinachokubalika katika soko ikiwemo nyama na maziwa na bidhaa zake mbalimbali,” amesema Mshigati.
 
Amesema TMDA imeshiriki kwenye Maonesho hayo kutoa elimu kwa wananchi na wadau mbalimbali wa kilimo na mifugo juu ya majukumu yake katika sekta ya dawa na Vifaa Tiba na kwamba moja ya jukumu lake ni kusimamia Dawa hizo na kuhakikisha wale wote wanaofanya bishara ya kuziuza wanafuata taratibu zilizowekwa.
 
Amewashauri wananchi kununua Dawa hizo kwenye maduka maalimu yaliyosajiliwa kisheria ambayo ndiyo yanatakiwa kuwa na wataalam wa dawa hizo na mifugo kwa ujumla sambamba na kufuata maelekezo ya wataalamu hao ili kuepuka kuleta madhara kwa mifugo na kukosa msaada wa kitaalamu pindi wanapotatizo.
Previous articleKINANA APIGA KURA KUCHAGUA VIONGOZI WA CCM OYSTERBAY
Next articleMKUU WA WILAYA YA KALAMBO ATEMBELEA BANDA LA BRELA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here