Home BUSINESS TIC IPO KUHUDUMIA WAWEKEZAJI WOTE WA NDANI NA NJE : MASHIBA

TIC IPO KUHUDUMIA WAWEKEZAJI WOTE WA NDANI NA NJE : MASHIBA

Meneja wa Kanda wa Kituo cha Uwekezaji (TIC) Kanda ya Nyanda za juu Kusini Venance Mashiba (kulia) akizungumza na mgeni aliyetembelea katika banda la Kituo hicho (hayumo pichani) kuelezea shughuli zinazofanywa na kituo hicho kwenye maonesho ya Nanenane yanayofanyika katika viwanja vya John Mwakangale Jijini Mbeya. (katikati) ni, Afisa Uwezehaji, Uwekezaji wa TIC Kanda ya Nyanda za juu Kusini Aljando Sindaro, na (kushoto) ni, Afisa Uhusiano na Mawasiliano wa TIC Robetha Makinda.

Meneja wa Kanda wa Kituo cha Uwekezaji (TIC) Kanda ya Nyanda za juu Kusini Venance Mashiba (wa pili kushoto) akiwa pamoja na watumishi wengine wa kituo hicho katika Maonesho ya Nanenane Jijini Mbeya

PICHA ZOTE NA: HUGHES DUGILO (MBEYA)

Na: Hughes Dugilo MBEYA.
Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kimesema kuwa sekta ya uwekezaji katika kuongeza thamani ya mnyoronyoro wa mazao imeendelea kukua hapa nchini kutokana na uwepo wa mwamko mkubwa wa wawekezaji wa ndani na nje ya nchi kuwekeza katika kilimo.
Hayo yamebainishwa na Meneja wa Kanda wa Kituo cha Uwekezaji (TIC) Kanda ya Nyanda za juu Kusini Venance Mashiba alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari Agost 3,2022 katika maonesho ya Nanenane yanayoendelea katika viwanja vya John Mwakangale Jijini Mbeya ambapo  TIC imeshiriki kwenye maonesho hayo kwa lengo la kutoa elimu kwa wananchi kufahamu shughuli mbalimbali zinazofanywa na Kituo hicho.
Mashiba amesema kuwa katika eneo la Nyanda za Juu kusini kuna fursa mbalimbali za uwekezaji katika kilimo, mifugo na uvuvi na kwamba kituo hicho kinaendelea kutoa elimu na kutangaza fursa za uwepo wa mnyororo wa thamani katika maeneo hayo ambapo kuna fursa kubwa katika uchakataji wa mazao hayo.
Aidha amesema kutokana na uwepo wa fursa katika maeneo ya kilimo, mifugo na uvuvi wanaendelea kutangaza fursa za uwekezaji katika kuzalisha pembejeo ambapo zinatumika katika kuongeza thamani mnyororo mzima wa uchumi kwenye meneo hayo.

“Wapo watu ambao waamini kwamba TIC ipo kwaajili ya kundi fulani la wawekezaji wakiwemo wale wa kutoka nje ya nchi tu, tunawaambia kituo hiki ni Taasisi ya Umma inayotoa huduma kwa wawekezaji wote wadogo kwa wakubwa, wa ndani na wa nje, kila mtu katika kundi lake anapata huduma stahiki katika kituo hiki ndio maana tupo hapa kutoa elimu na kuhamasisha wananchi kuona fursa zilizopo katika uwekezaji ili nao waweze kushikiri kulingana na fursa walizoiona” amesema Mashiba.

Katika hatua nyingine Mashiba amezungumzia uwepo wa mfumo wa kielekroniki wa taarifa za pamoja kutoka taasisi mbalimbali zinazomrahisishia mwekezaji kupata huduma bora na haraka katika dawati moja la kutoa huduma za mahala pamoja ili kumrahisisha mwekezaji kupata huduma zote za usajili katika dawati moja.

“Katika mfumo huu taasisi zote zinaunganisha mifumo yake ya utoaji hudumana kuwa katika mtandao mmoja ili mwekezaji anapokuja kwenye eneo moja kama vile (TIC) ataanzisha mahitaji yake ya uwekezaji kwa kuongea na (TIC) hivyo taarifa zake zitaenda kwenye taasisi zingine mbalimbali  kama vile BRELA, Uhamiaji, TRA, TBS, Wizara ya Viwanda na maeneo mengine bila yeye kutoka pale alipo,”. Amesema Mashiba

Amewahimiza wananchi kutembelea katika banda la TIC ili kupata elimu mbalimbali inayotolewa bandani hapo kuhusu shughuli mbalimbali za kituo hicho.

Previous articleMAGAZETI YA LEO JUMATANO AGOSTI 4-2022
Next articleNFRA YAKABIDHIWA MAGHALA YA KISASA YA KUHIFADHIA MAZAO KATAVI, SUMBAWANGA NA BABATI
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here