Home BUSINESS TANZANIA INA UTAJIRI MKUBWA WA BANDARI

TANZANIA INA UTAJIRI MKUBWA WA BANDARI

CACP Mwamini Rwamtali Kamanda wa Polisi Kikosi cha TAZARA akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kutembelea banda la Mamlaka ya Bandari Tanzania TPA katika Maonesho ya Nanenane 2022 yanayofanyika kitaifa kwenye viwanja vya John Mwakanganle jijini Mbeya ambapo kilele chake ni leo Jumatatu Agosti 8, 2022 zikihitimishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Rais Samia Suluhu Hassan. kushoto ni Kaimu Mkurugezi wa Idara ya Masoko na Uhusiano Mamlaka ya Bandari Tanzania TPA Bw. Nicodemus Mushi.

CACP Mwamini Rwamtali Kamanda wa Polisi Kikosi cha TAZARA akipokea zawadi kutoka kwa Upendo Mtinangi Afisa Mafunzo Chuo cha Bandari mara baada ya kutembelea banda la Mamlaka ya Bandari Tanzania TPA katika Maonesho ya Nanenane 2022 yanayofanyika kitaifa kwenye viwanja vya John Mwakanganle jijini Mbeya ambapo kilele chake ni leo Jumatatu Agosti 8, 2022.

CACP Mwamini Rwamtali Kamanda wa Polisi Kikosi cha TAZARA akisikiliza maelezo kutoka kwa Kaimu Mkurugezi wa Idara ya Masoko na Uhusiano Mamlaka ya Bandari Tanzania TPA Bw. Nicodemus Mushi wakati alipotembelea banda la Mamlaka ya Bandari Tanzania TPA katika Maonesho ya Nanenane 2022 yanayofanyika kitaifa kwenye viwanja vya John Mwakanganle jijini Mbeya ambapo kilele chake ni leo Jumatatu Agosti 8, 2022 zikihitimishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Rais Samia Suluhu Hassan. 

CACP Mwamini Rwamtali Kamanda wa Polisi Kikosi cha TAZARA akiuliza swali kwa Kaimu Mkurugezi wa Idara ya Masoko na Uhusiano Mamlaka ya Bandari Tanzania TPA Bw. Nicodemus Mushi alipotembelea banda la Mamlaka ya Bandari Tanzania TPA katika Maonesho ya Nanenane 2022 yanayofanyika kitaifa kwenye viwanja vya John Mwakanganle jijini Mbeya.

Wafanyakazi wa Bandari wakiwa katika banda lao. 

Baadhi ya wananchi wakitembelea katika banda hilo.

MBEYA.

Tanzania ina utajiri mkubwa wa Bandari ambao watu wengi hawauelewi jambo ambalo ni muhimu shirika la Bandari Tanzania TPA kuendelea kushiriki maonesho kama haya na kuelimisha watu mbalimbali ili wawe na uelewa wa kutosha kuhusu bandari zetu na shughuli zinazofanya.

Akizungumza mara baada ya kutembelea banda la Mamlaka ya Bandari Tanzania CACP Mwamini Kamanda wa Polisi Kikosi cha TAZARA amesema taarifa niliyopewa na maofisa wa bandari wakati alipotembelea banda hilo inaonyesha jinsi nchi ilivyo na utajiri mkubwa wa bandari nchini kote

“Nimeniambia kuwa Tanzania ina bandari karibu 600 kubwa na ndogondogo lakini watu wengi wanajua Bandari ya Dar es Salaam, Mtwara na Tanga pekee jambo ambalo linaifanya jamii kutoelewa vizuri shughuli za bandari,” Amesema Afande Mwamini.

Ameongeza kuwa mimi binafsi nilikuwa nakijua chuo cha bandari kule Temeke ambacho sikujua hata kinafanya nini lakini nimepata uelewa kuwa chuo hicho ni muhimu na kinatoa mafunzo mazuri kwa vijana wa kitanzania katika elimu ya kati kuhusu masuala ya shughuli mbalimbali za kibandari ambayo inaweza kuwasaidia kupata ajira na maisha yao kwenda vizuri kiuchumi katika familia zao.

Maonesho ya Nanenane 2022 yanayofanyika kitaifa kwenye viwanja vya John Mwakangale mkoani Mbeya yamefikia kilele chake leo Jumatatu Agosti 8, 2022 ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan ameyafunga rasmi.

Previous articleTPA YATOA ELIMU KWA WANANCHI MAONESHO YA NANENANE MBEYA
Next articleTASAC KICHOCHEO AJENDA YA 10/30, YAWATAKA WANANCHI KUENDELEA KUTUMIA BANDARI
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here