Home BUSINESS SIDO , NELICO & PACT WATOA MAFUNZO YA VITENDO KWA WAJASIRIAMALI MANISPAA...

SIDO , NELICO & PACT WATOA MAFUNZO YA VITENDO KWA WAJASIRIAMALI MANISPAA YA SHINYANGA

Afisa Uendelezaji Biashara SIDO Mkoa wa Shinyanga, Joseph Taban (wa pili kulia) na Meneja wa SIDO Mkoa wa Shinyanga, Hopeness Eliya wakionesha sabuni zilizotengenezwa na wajasiriamali waliopatiwa mafunzo ya vitendo kwa muda wa siku 8. Aliyevaa suti nyeusi ni mgeni rasmi wakati wa kufunga mafunzo hayo, Simeo Makoba ambaye ni Meneja wa Vipindi na Mhariri Mkuu wa Redio Faraja Fm. Kulia ni Afisa Uchumi kutoka shirika la NELICO, Fortunatus Richard akifuatiwa na Afisa Uhusiano Radio Faraja, Getrude Thomas. Wa kwanza kushoto ni mmoja wa wajasiriamali hao Suzana Nuhu.
 
Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO) Mkoa wa Shinyanga kwa kushirikiana na New Light Children Center Organization (NELICO) na Shirika la PACT Tanzania wametoa mafunzo ya vitendo (utengenezaji wa sabuni, batiki na vifungashio) kwa wajasiriamali 40 kutoka kata za Ngokolo,Chamaguha, Ndala na Kambarage Manispaa ya Shinyanga kwa lengo la kuwajengea uwezo ili waweze kujiajiri na kuajiri wengine huku wakiinua uchumi wa familia na taifa kwa ujumla.
 
Mafunzo hayo yaliyofanyika kwa siku 8 katika ukumbi wa SIDO Mkoa wa Shinyanga yamefungwa leo Alhamisi Agosti 18,2022 na Meneja wa Vipindi na Mhariri Mkuu wa Kituo cha Matangazo Radio Faraja Fm Stereo, Simeo Makoba.
 
Akizungumza wakati wa kufunga mafunzo hayo yaliyohusisha wanawake 39 na mwanaume mmoja, Makoba ameishukuru SIDO, NELICO na PACT Tanzania kwa kutoa mafunzo ya vitendo bure kwa wajasiriamali hao ambayo yatawasaidia kujiinua kiuchumi.
 
“Mmepata mafunzo haya nendeni mkatumie ujuzi mliopata kuanzisha viwanda vidogo ili mjiajiri na kuajiri wengine. Nimeo ana bidhaa mlizotengeneza ni za viwango vya hali ya juu. Kazalisheni bidhaa kwa viwango na ubunifu ili mpate masoko mazuri. Ubora wa bidhaa yako ndiyo utakuweka sokoni”,amesema Makoba.
 
Makoba ametumia fursa hiyo kuwataka wajasiriamali kupitia vikundi kuchangamkia mikopo inayotolewa na serikali kwenye Halmashauri za wilaya.


</d…

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here