Home BUSINESS RIPOTI ZA TEITTI ZAWAVUTIA WASHIRIKI WA MAONESHO YA NANENANE JIJINI MBEYA

RIPOTI ZA TEITTI ZAWAVUTIA WASHIRIKI WA MAONESHO YA NANENANE JIJINI MBEYA

Katika kuhitimisha kilele cha Sikukuu ya Wakulima Kitaifa Nane Nane ripoti za ulinganishi wa malipo ya Kampuni za Madini, Mafuta na Gesi Asilia na Mapato ya Serikali zinazoandaliwa na Taasisi ya  Uhamasishaji Uwazi na Uwajibikaji katika rasilimali Madini, Mafuta na Gesi Asilia zimekuwa kivutio kikubwa kwa washiriki mbalimbali wa maonesho hayo.

Imeelezwa kuwa tangu Tanzania imejiunga katika umoja wa Kimataifa wa Uwazi na Uwajibikaji, TEITI hadi hivi sasa imeshakamilisha kutoa jumla ya Ripoti zake (12) ambapo Uwazi umeimarika tofauti na hapo ilivyokuwa awali.

Aidha, TEITI imefafanua kuwa itaendelea kutekeleza vigezo vya Kimataifa vya Uwazi na Uwajibikaji vya EITI na Sheria ya TEITA pamoja na kanuni zake kikamilifu ili kuimarisha Uwazi na Uwajibikaji katika usimamizi wa rasilimali Madini,  Mafuta na Gesi Asilia Tanzania.

Hata hivyo wananchi mbalimbali kutoka ndani na nje ya Jiji la Mbeya walijitokeza na kupata fursa ya kujifunza mambo mbalimbali yanayofanywa na TEITI katika maonesho hayo. 

Maonesho ya Wakulima Kitaifa Nanenane, yalianza tarehe 1 hadi 8 Agosti, 2022 yenye kauli mbiu “Agenga ya 10/30 “Kilimo ni Biashara, Shiriki kuhesabiwa kwa Mipango Bora ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi” yaliyofikia kilele chake tarehe 8 Agosti 2022 na kufungwa rasmi na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia  Suluhu Hassan katika viwanja vya John Mwakangale Jijini Mbeya.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here