Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhe. Martin Shigella akikagua hatu za ujenzi wa Jengo la ofisi za Halmashauri ya Wilaya ya Nyang’hwale
Wakwanza kushoto ni kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Nyang’hwale Rajabu Mmunda
Kati kati ni Mkuu wa wilaya ya Nyang’hwale Mhe. Jamhuri Devoid akizungumza mbele ya Mkuu wa mkoa wa Geita Mhe. Martin Shigella
Mkuu wa mkoa wa Geita Mhe, Martin Shigella akizungumza baada ya kukagua ujenzi wa Jengo la ofisi ya Halmashauri ya wilaya ya Nyang’hwale.
Na: Costantine James, Geita.
Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhe, Martin Shigella ameshangazwa na kasi ya ujenzi wa jengo la ofisi ya Halmashauri ya wilaya ya Nyang’hwale mkoani Geita kutokamilika kwa wakati licha ya serikali kutoa pesa za ujenzi wa jengo hilo.
Mhe, Shigella amebainisha hayo tarehe 18.8.2022 katika ziara yake wilayani Nyang’hwale akiambatana katibu tawala mkoa wa Geita Prof. Godius Kahyarara pamoja na kamati ya ulinzi na usalama ngazi ya mkoa kwenye ziara ya kikazi pamoja na kujitambulisha kwa viongozi na watumishi wa wilaya ya Nyang’hwale.
Shigella amesema matarajio ya ofisi hiyo mpaka sasa ingekuwa imeshakamilika na kuanza kutumika kama ilivyo kusudiwa lakini bado ujenzi huo unasuasua kutokana na sababu mbalimbali.
Amesema kasi ya ujenzi wa jengo hilo haulidhishi hivyo amemtaka mkandarasi amnaesimamia ujenzi wa jengo hilo SUMA JKT kuongeza kasi ya ujenzi ili kuweza kukamilika kwa haraka na lianze kutumika kama ilivyo kusudiwa.
Mhe shigella amemuagiza mkandarasi anaesimamia ujenzi huo ambae ni SUMA JKT kuhakikisha kuhakikisha ujenzi ndani ya mwaka huu wa fedha 2022/2023 unafikia asilimia 95% sambamba na kukamilisha baadhi ya maeneo katika jengo hilo ili yaanze kutumika.
Mkuu wa wilaya ya Nyang’hwale Mhe, Jamhuri Devid amekiri mradi huo kuchukua mda mrefu kinyume na mda uliotarajiwa kukamilika hali inayosababisha viongozi mbalimbali wa halamashauri ya Nyang’hwale kuendesha shughuli zake katika hospitali ya wialaya.
Mhe, Jamhuri amesema ujenzi wa jengo hilo unatakiwa kukamilika haraka ili kuwezesha Mkurungezi wa halsmashauri hiyo kuhamia katika jengo na kupisha katika jengo la hospitali ya wialya ya ili litumike kwa mahitaji ya hospitali.
Amesema licha ya ukamilishwaji wa jengo hilo pia kuna haja ya kufanya ukaguzi wakina juu ya fedha zilizotumika katika matumizi ya utakelezaji wa mradi huo.
Awali kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Nyang’hwale Rajabu Mmunda wakati akaisoma taarifa ya ujenzi wa jengo hilo mbele ya mkuu wa mkoa Mhe, Martin Shigella amesema ujenzi wa jengo hilo ulianza kutekelezwa mwaka 2017 unaulitarajiwa kukamilika mwaka 2019 kwa gharama ya bilioni 4.1.
Amesema mpaka sasa ujenzi wa jengo hilo umefikia asilimia 67% ambapo zaidi ya bilioni 1.9 zimeshatumika katika utekelezaji wa ujenzi wa jengo hilo.
Amesema changamoto zilizopelekea kusuasua kwa ujenzi wa jengo hilo ni pamoja na kuchelewa kwa mchoro katika hatua za mwanzo, ujenzi wa msingi kukamikika kwa kusuasua kutokabna na fedha zake kutumika katika matumzi mengine.