Home BUSINESS PROGRAMU YA KUTAMBUA HALI YA AJIRA KWA WAHITIMU KATIKA VYUO VYA VETA...

PROGRAMU YA KUTAMBUA HALI YA AJIRA KWA WAHITIMU KATIKA VYUO VYA VETA NCHINI YALETA MAFANIKIO

Asibatike William Mwalimu kutoka Chuo cha VETA Mbeya akielezea hali ya ajira kwa wahitimu wa ufundi stadi nchini alipozungumza katika Maonesho ya Kilimo-Nanenane yanayofanyika Kitaifa kwenye viwanja vya John Mwakangale mkoa wa Mbeya. kulia ni Jofrey Nyandindi Mchambuzi wa Nguvu kazi na Msoko Kanda ya Kusini Magharibi kutoka VETA.

 Asibatike William Mwalimu kutoka Chuo cha VETA Mbeya akitoa maelezo kwa mwananchi aliyetembelea katika banda hilo katika Maonesho ya Kilimo-Nanenane. (PICHA NA: HUGHES DUGILO)

NA: Hughes Dugilo, MBEYA.

Imeelezwa kuwa Programu ya Ufuatiaji wa wahitimu katika Vyuo vya Ufundi vilivyopo chini ya Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) inayowezesha kutambua hali ya ajira kwa wahitimu wanaomaliza mafunzo yao katika vyuo hivyo,  imewezesha kuwatambua wahitimu wa Vyuo hivyo mahala walipo na kazi wanazofanya.

Programu hiyo ya ufuatiliaji wahitimu (tracer Study) inafanyika kila baada ya miaka mitano yenye lengo la kufanya tathimini juu ya ubora wa mafunzo yanayotolewa.

Akizungumza katika mahojiano maalum ndani ya Banda la VETA kwenye Maonesho ya Nanenane yanayoendelea Kitaifa katika viwanja vya John Mwakangale Jijini Mbeya  mwalimu kutoka Chuo cha Veta MBEYA Asibatike William amesema kuwa Programu hiyo imeweza kupata takwinu sahihi za Maendeleo ya wahitimu katika soko la ajira.

“Programu hii inaonesha hali ya Ajira kwa wanafunzi tulikuwa tunawadahili kwenye Vyuo vyetu kujua nani yuko wapi na anafanya” amesema Mwl. Asibatike.

Ameongeza kuwa kufuatia Programu hiyo jumla ya asilimia 75 ya wahitimu wamepata ajira, ambao kati ya hao  asilimia 32 ya wahitimu katika Vyuo vya VETA wameajiriwa katika maeneo mbalimbali ikiwemo viwandani na asilimia 38 wamejiajiri wenyewe.

“Takwimu hizi kwetu sisi VETA ni muhimu sana kwani zinatusaidia kufanya ufuatiliaji na kujipima na kuweka mipango ya baadae ikiwemo kuongeza mbinu za ufundishaji ili kukidhi matwaka ya soko ameongeza.


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here