Home BUSINESS NIC YATAMBULISHA BIMA YA MAZAO KWA WADAU WA KILIMO MAONESHO YA NANENANE...

NIC YATAMBULISHA BIMA YA MAZAO KWA WADAU WA KILIMO MAONESHO YA NANENANE JIJINI MBEYA

Meneja wa Shirika la Bima la Taifa (NIC) Mkoa wa Mbeya Justine Seni (wa tatu kulia) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watumishi wa Shirika hilo kwenye Banda lao katika maonesho ya Nanenane yanayofanyika Kitaifa katika Viwanja vya John Mwakangale Jijini Mbeya.

Wakala wa Bima wa NIC Chrisostme Haule ((kulia) akimuhudumia Mteja aliyefika kupata huduma za Bima kwenye Maonesho hayo.

Meneja wa Shirika la Bima la Taifa (NIC) Mkoa wa Mbeya Justine Seni (kushoto) akiwa na Afisa Maendeleo ya Biashara Mwandamizi wa Shirika hilo Alex Suzuguye (kulia) wakifurahia jambo katika Banda lao.

 (PICHA ZOTE NA: HUGHES DUGILO)

Na: Hughes Dugilo, Mbeya.
Shirika la Bima la Taifa (NIC) limetumia kiasi cha fedha za Kitanzania zaidi ya Shilingi milioni 500 kama malipo ya Bima ya Mazao kwa  wakulima waliopatwa na majanga yaliyopelekea kuharibika kwa mazao yao Shambani.

Akizungumza kwenye mahojiano maalum leo Agosti 1,2022 katika Maonesho Nanenane yanayofanyika Kitaifa Jijini mbeya, Meneja wa NIC Mkoa wa Mbeya Justine Seni amesema kuwa wakulima na wafugaji wamenufaika na Bidhaa hiyo toka ilipoingizwa sokoni na kwamba Shirika linaendelea kutoa elimu na kuwahamasisha wadau katika sekta ya kilimo na mifugo kutumia fursa ya uwepo wa Bima hiyo na kujiunga nayo ili kujihakikishia usalama wa mazao yao.

“Bima hii ya kilimo kwa sasa inafanya vizuri sana sokoni toka tulipoianzisha imekuwa ni msaada kwa wakulima wetu na wafugaji na tayari tumeshatoa zaidi ya Milioni 500 kwa mwaka uliopita. Hapa nanenae tumekuja kushiriki lakini pamoja na mambo mengine pia tunaendelea kuiuza hii bidhaa ili wakulima wengi wapate kujiunga na kupata uhakika wa usalama wa mazao yao” amesema Seni.

Ameainisha maeneo ambayo mkulima anaweza kunufaika na Bima hiyo ni pamoja na ukame, mafuriko, magonjwa na wadudu wasiodhibitika au kutibika, vimbunga na Mvua ya mawe. Pia amesema kuwa Shirika litaendelea kushirikiana na wadau wa sekta ya kilimo na mifugo kuhakikisha malipo ya fidia zao yanapatikana kwa haraka kama ilivyo kawaida ya Shirika hilo katika kulipa waathirika wa majanga mbalimbali.

Naye Afisa maendeleo ya Biashara Mwandamizi wa NIC Alex Suzuguye amesema kuwa Shirika hilo limefanikiwa kuwafikia wakulima zaidi ya 500 waliojunga na Bima hiyo na kwamba vipo vyama vya Ushirika zaidi ya 200 vilivyopo katika mikoa mbalimbali ambavyo wakulima wao pamoja na wafugaji wamejiunga na Bima hiyo.

Aidha amesema kuwa wakulima walionufaika na Bima hiyo ni pamoja na wakulima wa Mpunga katika Mkoa wa Mbeya, wakulima wa Mpunga na Miwa katika Mkoa wa Morogoro, wakulima wa Korosho katika mikoa ya Kusini, na mazao mengine yanayozalishwa katika mikoa mbalimbali hapa nchini.

“Sisi kama Bima tumeendelea kutoa huduma hii na kwakua ni Shirika la Serikali ndio tumepewa dhamana ya kuhakikisha wakulima wetu mazao yao wanalindwa na kwamba kilimo chao kiwe chenye tija wasipate hasara pale wanapopatwa na matatizo” ameongeza Suzuguye. Na kuongeza kuwa.

“Mpaka sasa hakuna malalamiko yoyote kutoka kwa wakulima wote na wafugaji waliojiunga na Bima hii, wamekuwa wakiipongeza Serikali na Shirika lao kwa kuanzisha Bima hii” ameongeza.

uduma hii na kwakua ni Shirika la Serikali ndio tumepewa dhamana ya kuhakikisha wakulima wetu mazao yao wanalindwa na kwamba kilimo chao kiwe chenye tija wasipate hasara pale wanapopatwa na matatizo” ameongeza Suzuguye. Na kuongeza kuwa.


“Mpaka sasa hakuna malalamiko yoyote kutoka kwa wakulima wote na wafugaji waliojiunga na Bima hii, wamekuwa wakiipongeza Serikali na Shirika lao kwa kuanzisha Bima hii” ameongeza Suzuguye. Na kuongeza kuwa


“Mpaka sasa hakuna malalamiko yoyote kutoka kwa wakulima wote na wafugaji waliojiunga na Bima hii, wamekuwa wakiipongeza Serikali na Shirika lao kwa kuanzisha Bima hii” ameongeza.
Previous articleMAGAZETI YA LEO JUMATATU OGASTI 1-2022
Next articleMAGAZETI YA LEO JUMANNE OGASTI 2-2022
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here