Afisa Mwandamizi Maendeleo ya Biashara wa NIC Alex suzuguye (kulia) aliyesimama akizungumza na waandishi wa habari (hawamo pichani) katika mahojiano maalum ndani ya Banda lao kwenye Maonesho ya Nanenane Jijini Mbeya. pamoja nae ni, Ephrasia Mawalla Afisa Uhusiano na Mawasiliano NIC (katikati aliyekaa) na Catherine Majigwa Afisa Bima wa NIC (Kushoto) aliyekaa.
Afisa Mwandamizi Maendeleo ya Biashara wa NIC Alex suzuguye akionesha baadhi ya wateja waliokata Bima za NIC
Afisa Mwandamizi Maendeleo ya Biashara wa NIC Alex suzuguye akitoa ufafanuzi Juu ya aina za Bima wanazozitoa. (PICHA NA: HUGHES DUGILO – MBEYA)
Na: Hughes Dugilo, MBEYA
Shirika la Bima la Taifa NIC limeendelea kujiimaeisha kiuchumi kwa kuwekeza katika Amana za mabenki mbalimbali hapa nchini na hati fungani na kupelekea Shirika hilo kutokuwa na tatizo la Ukwasi.
Hayo ya mmeelezwa na Kaimu Afisa Mwandamizi Maendeleo ya Biashara wa Shirika hilo Alex Suzuguye alipokuwa akizungumza kwenye mahojiano maalum na waandishi wa habari katika Banda lao kwenye Maonesho ya Nanenane yanayoendelea Kitaifa katika viwanja vya John Mwakangale Jijini Mbeya.
Suzuguye ameelekeza kuwa wananchi wanapaswa kufahamu ukubwa wa Shirika lao kiuchumi Ili waendelee kujenga imani kwani kwa sasa Shirika hilo limekuwa kimbilio kwa wananchi wengi kujitokeza kujiunga katika huduma za Bima mbalimbali zinazotolewa na Shirika hilo.
Ameongeza kuwa uwezo wa Ukwasi wa Shirika hilo limepelekea kulipa fidia mbalimbali za Bima kwa wakati ambapo ndani ya siku chache Mtu anakuwa ameshalipwa madai yake.
“Kitu cha kwanza ambacho mtu anatakiwa kufanya anapotaka kujiunga na Kampuni ya Bima lazima aangalie uwezo wa kifedha wa Kampuni husika sasa kwa hapa nchini ukizungumzia taasisi ya Bima yenye uwezo mkubwa wa kifedha unazungumzia NIC ukiangalia katika kipindi cha miaka mitatu Shirika limeweza kufanya vizuri sana kwa mfano kwa mwaka wa fedha uliopita liliweza kutengeneza faida zaidi ya Bilioni 70 na kuwa Kampuni ya Bima iliyotengeneza faida kubwa kuliko Kampuni yoyote ya Bima hapa nchini” ameeleza Suzuguye.
Ameongeza kuwa mafanikio hayo yametokana na imani kubwa waliyonayo wananchi kwa Shirika lao kwa kutambua umuhimu wa kuwa na Bima katika shughuli zao pamoja na wawekezaji na wafanyabiashara kutoka nje ambao wamekuwa wakikatia Bima miradi yao kutokana na uwezo mkubwa wa kifedha wa Shirika hilo.
Aidha Suzuguye ameelezea eneo la uwekezaji uliofanywa na Shirika hilo ambapo amesema kuwa kwa mwaka wa fedha uliopita Shirika limewekeza zaidi bilioni 120 na kwamba mpasa sasa mfuko una thamani wa zaidi ya Shilingi Bilioni 400.