Mkurugenzi wa Masoko na Huduma kwa Wateja wa Shirika la Bima la Taifa (NIC) Yessaya Mwakifulefule akizungumza katika mahojiano maalum na Kituo cha habari cha Chanel 10 katika Banda lao kwenye Mzonesho ya Nanenane yanayoendelea katika Viwanja vya John Mwakangale Jijini Mbeya.
Mkurugenzi wa Masoko na Huduma kwa Wateja Shirika la Bima la Taifa (NIC) Yessaya Mwakifulefulewa (wa tano kutoka kushoto na kulia) akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Shirika hilo katika maonesho hayo. PICHA NA HUGHES DUGILO
Na: Hughes Dugilo, MBEYA.
Shirika la Bima la Taifa (NIC) limeendelea kutoa elimu kwa wananchi mbalimbali juu ya huduma za Bima wanazozitoa kwa wanaotembelea katika maonesho ya Kilimo ya Nanenane yanayoendelea katika viwanja vya John Mwakangale Jijini mbeya.
Akizungumza katika Maohojiano maalum na waandishi wa habari katika Banda la Shirika hilo Mkurugenzi wa Masoko na Huduma kwa Wateja wa Shirika hilo Yessaya Mwakifulefule amesema kuwa ushiriki wao kwenye maonesho hayo yanatoa fursa kwa wananchi wanaotembelea hususani wadau wa kilimo kufahamu huduma za Bima mbalimbali zinazotolewa na Shirika hilo ikiwemo Bima ya mazao ambayo imekuwa mkombozi kwa wakulima hapa nchini.
“Tupo hapa kwenye maonesho ya Nanenane tunataka watanzania wote kwa ujumla kufahamu Huduma zetu za Bima, kwa wakulima wakubwa kwa wadogo ilimradi tu awe ana shamba lake kuanzia heka moja kwenda juu waje wakatie Bima mazao yao na mifugo yao ili ikitokea wanapata majanga waweze kulipwa fidia zao. Hakuna haja ya kuwa na hofu kama ni kuharibika kwa mazao au kufa kwa mifugo NIC ipo tuletee sisi hizo ‘stress’ zako za kibiashara tukae nazo sisi wewe baki na maisha ya amani” amesema Mwakifulefule.
Amesisitiza kuwa Shirika hilo limeendelea kujiimarisha katika kuwafikia wakulima wengi kwa kuwapa elimu juu ya uwepo wa Bima hiyo ambapo amebainisha uwepo wa kikosi kipana cha vijana wenye weledi na ujuzi mkubwa katika kutoa huduma za Bima pamoja na timu nzima ya elimu kwa umma iliyowezesha kuwafikia wananchi wengi kufahamu Huduma zao.
“kuna mwamko mkubwa sana wa vijana kujihusisha na kilimo na NIC tunaungana na Serikali yetu katika kuhakikisha tunaunga mkono jitihada za kuwahusisha vijana katika kilimo.Tumemsikia Mhe. Waziri Mkuu akisisitiza kuwafikia vijana wengi, na sisi tuko tayari kuwafia na kuwahamasisha huku tukiwaelimisha juu ya Bima hii ya mazo ili wawe na uhakika wa kazi zao kwani sisi ndo BIMA” amesisitiza.
Maonesho ya Kilimo Nanenane maka huu yamekuwa kivutio kikubwa kwa wananchi wa Jiji la Mbeya na mikoa ya Nyanda za Juu Kusini kwa ujumla ambapo Shirika la Bima la Taifa NIC limeweka kambi katika Maonesho hayo huku likiwa na kikosi kazi kutoka katika Idara tofauti kikiongozwa na Idara ya Masoko chini ya usimamizi wa Mkurugenzi wake Yessaya Mwakifulefule. #SISI NDIO BIMA#