Home LOCAL MUSWADA WA SHERIA YA USIAMAMIZI WA MAAFA WAWASILISHWA KWA KAMATI

MUSWADA WA SHERIA YA USIAMAMIZI WA MAAFA WAWASILISHWA KWA KAMATI

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. George Simbachawene akizungumza katika kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria wakati ofisi hiyo ikiwasilisha   Muswada wa Sheria ya Usimamizi wa Maafa kilichofanyika Agosti 30, 2022 Ukumbi wa Bunge, Jijini Dodoma.

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Ummy Nderiananga akiwasilisha Muswada wa Sheria ya Usimamizi wa Maafa mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria Agosti 30, 2022 Ukumbi wa Bunge, Jijini Dodoma.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Joseph Mhagama akieleza jambo wakati wa kikao cha kamati hiyo kilichofanyika katika ukumbi wa Bunge, Agosti 30, 2022 Jijini Dodoma.

Mbunge wa Jimbo la Manyoni Mashariki Mhe. Yahaya Masare  (katikati) akichangia hoja wakati wa kikao hicho.

(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)

Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu imewasilisha Muswada wa Sheria ya Usimamizi wa Maafa kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria.

Kikao hicho kilihusisha viongozi mbalimbali  kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu akiwemo Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu  anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene, na Naibu Waziri wake  Mhe. Ummy Nderiananga. Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo Dkt. John Jingu pamoja na  Naibu wake Bwa. Kaspar Mmuya.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here