Home LOCAL MUST YANG’ARA NANENANE KITAIFA 2022

MUST YANG’ARA NANENANE KITAIFA 2022

Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya kimeshika  nafasi ya kwanza kitaifa katika  maonesho ya nanenane kitaifa katika viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya.

Maonesho hayo ambayo yameshirikisha wakulima binafsi, majeshi ya ulinzi na usalama, mabenki na taasisi na taasisi za elimu ya juu vikiwemo vyuo vikuu.

MUST imejizolea point nyingi zaidi na kushika nafasi ya kwanza katika kundi la taasisi za elimu ya juuu, ikifuatiwa na Chuo kikuu cha Dar es salam na Taasisi ya Uhasibu Tanzania.

Maonesho ya nanenane kitaifa kwa mwaka 2022, yamefanyika kitaifa Mkoani Mbeya ambapo Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania MHE. Dkt. Isdori Mpango aliyafungua rasmi tarehe 1 Agost 2022, na kufungwa rasmi leo tarehe 8 Agosti 2022 na MHE. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here