Home BUSINESS KIJIJI CHA NYUKI SINGIDA NA FURSA ZAKE

KIJIJI CHA NYUKI SINGIDA NA FURSA ZAKE

Na: Mwandishi wetu

KIJIJI cha Nyuki kilichopo mkoani  Singida ni miongoni eneo ambalo,linafuga nyuki kupitia vitalu mbalimbali na limekuwa ni miongoni mwa kivutio kwa watu mbalimbali wa ndani na nje ya mkoa huo.

Kijiji hichi kimekuwa ni kijiji mfano kwa watu mbalimbali ambao wanakuwa wanatamani kuingia katika ufugaji wa nyuki ambapo uwapatia mafunzo ya kuonesha ni namna gani wanaweza kufuga nyuki kwa njia iliyosalama na rahisi.

Pia kijiji hicho kimekuwa kikipokea wageni mbalimbali ambao kwa asilimia kubwa wamekuwa wanatembea na kujionea namna ya nyuki wanavyofugwa na kuweza kutembeza katika maeneo mbalimbali.

Kuna umuhimu mkubwa wa ufugaji wa nyuki kwa binadamu kwani inawasaidia kwa kiasi kikubwa kupata mazao yake ambayo upelekea mtu kupata fedha.

Na hili ufugaji huu wa nyuki uwe katika kiwango kikubwa ni vema wafugaji  wa nyuki  kuacha dhana ya kuelewa kuwa nyuki wanamazao mawili  tu ya asali na nta wakati wanamazao mengine matano yenye thamani kubwa.
 
Miongoni mwa mazao hayo ni pamoja na  Gundi ambayo bei yake kwa kilo ni sh.150,000, maziwa sh.milioni 4 kwa lita, chamvua sh.300, 000 kwa kilo,supu ya nyuki sh.50,000 kwa lita na sumu ya nyuki sh.400,000 kwa gramu.

Suphian Nkuwi,Afisa Habari na Masoko wa Kijiji cha Nyuki Singida, anasema kijiji hicho ni miongoni mwa vijiji vyenye mafanikio makubwa katika jamii.

Anasema  ni vema watu wakakaribia katika ufugaji huo wa nyuki na kujifunza mambo mbalimbali kutoka katika kijiji hicho ambacho kwa asilimia kubwa kimefanya vizuri katika ufugaji wa nyuki.

”Karibuni tufuge nyuki kuunga mkono juhudi za  Serikali ya awamu ya Sita  Rais Samia  Suluhu Hassan ya kuboresha Sekta ya Ufugaji kama ambavyo Sera ya Taifa ya Ufugaji nyuki ya Mwaka 1998 inavyohimiza,”anasema na kuongeza

”Sera hiyo inahimiza uanzishwaji wa hifadhi za nyuki za Serikali Kuu, Serikali za Mitaa na watu binafsi ili kulinda makundi ya nyuki pamoja na malisho yao,hivyo Kijiji cha Nyuki kimeweza fanikiwa kuunga mkono katika sera hiyo,”anasema

Aidha anasema  kulingana na takwimu za Shirika la Chakula Duniani(FAO),Tanzania ni nchi ya pili  kwa ufugaji nyuki Afrika baada ya Ethiopia,hivyo kuna umuhimu wa watanzania kuamka na kuanza kufuga nyuki kwa wingi na kisasa.

Anasema ni jamii ikaona fursa hii iliyopo  kupitia Kijiji cha Nyuki Singida, kuweza kuiendeleza kwa vitendo na kwenda kujifunza zaidi juu ya umuhimu wa ufugaji wa nyuki na mazao yake ili kuifanya Tanzania  kuwa Nchi ya kwanza Afrika kufuga nyuki.

”Natoa wito kwa Watanzania kujitokeza kwa wingi kuja kijiji cha nyuki hapa  Singida na kujionea namna ya nyuki wanavyofugwa,faida zake,umuhimu wake wa kufugwa pamoja na kujua ni namna gani unaweza kujiingizia kipato kupitia zao hilo la nyuki,”anasema na kuongeza

”Mimi nilikuja tu kwenye mapumziko nikapata bahati ya kuja kutembelea Kijiji hiki,ambapo kiukweli pamoja na mwaliko ila sikudhani kama kuna cha kunikonga moyo humo ndani ya kijiji hicho ,ukizingatia sikuwahi kwenda hata mara moja licha ya kupasikia sikia na kumsikia Mwekezaji Mwanzilishi, Kiemi nashukuru nimejifunza mengi katika kijiji hicho,”anasema
 
Anasema kuwa Kijiji cha nyuki ni Shule, Hospitali, Kiwanda, Sehemu ya Utalii, Hifadhi, Soko , Hoteli na Ujumla wa Mambo mengine ya kawaida kwa Binadamu. ” Mimi na watalii wengine niliowakuta hapo juu tulipata mazao ya Nyuki na huduma zingine katika Kijiji cha Nyuki  na kujifunza vitu vingi ikiwemo uwepo wa Asali Asilia isiyokuwa na  mchanganyiko wowote wa kitu kisichofaa,Vumbi la Singida ni  Bidhaa inayojulikana kama “Only nature complete food” au “Miracle or Magic food,Mishumaa ya nta,Sumu ya Nyuki pamoja na Gundi ya Nyuki.

Pia anasema ameweza kujionea Maziwa nyuki pamoja na Supu ya Nyuki
ambayo inatokana na  zao la nyuki watoto au larvae lina protini nyingi.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji Kijiji cha Nyuki,Philemon  Kiemi anasema mipango waliyonayo ni kutangaza Kijiji cha nyuki ni kupitia kuzalisha Mazao ya nyuki na kutoa huduma  zenye Viwango vya juu na vinavyokubalika duniani kote.

Anasema wageni wapokwenda katika  kijiji cha nyuki watakutana na Mazao yote ya nyuki na huduma zote za nyuki pia  vitu vya kitalii kama  sehemu za kulala wageni ambazo ni Hema , Bwawa la kuogelea, Hoteli inayopika vyakula vya Asili  ya Singida, Makumbusho ya nyuki , Shule ya nyuki kwa vitendo , Viwanja vya Michezo ya aina mbalimbali , Maktaba ya Kijiji cha nyuki , Viwanda vya kuchakata Asali asilia, Vumbi la Singida, Gundi ya nyuki, Sumu ya nyuki, Maziwa ya nyuki, Nta ya nyuki na Mazao mengineyo.

”Watalii na watu wanaoingia humu wana fursa ya kuvuna na kuyatumia mazao haya ya nyuki wakiwa ndani ya Kijiji cha nyuki,sisi tunafahamu Watanzania wanahitaji Mabadiliko katika nyanja nyingi ikiwemo namna ya kulala, kula na kuvaa,pia wanahitaji  vitu vipya na kubadili mtazamo kwa jinsi walivyokuwa wanatibiwa, wanasoma na wanapata Utajiri,”anasema na kuongeza

”Vijana wote wanaotembea na Bahasha na wale wanaondelea kusoma , wawekeze akili zao kwenye Misitu na nyuki ili tuweze kutoa mali zilizopo msituni , kuzileta kwenye soko na Tutajirike na kuanzisha Familia zenye Furaha, maisha yenye furaha na Kufanyia kazi Mazingira yanayofurahisha,”anasema

Anasema gharama za mafunzo ni sh.Milioni moja   kwa mwezi ikihusisha malazi na chakula, Gharama za kutembelea kwa siku ni 50’000, Gharama za kutumia ” IFONEO -Safari Lodges and Beach resorts  100’000 kwa Siku.

Anasema mbali na vivutio vya nyuki kuna vivutio vingi katika mkoa wa Singida ambavyo ni  Wahadzabe waishio porini, Bwawa la maji ya moto, Jiwe linalocheza, Vyakula na mtunda yenye asili ya Singida, Kuongelea na kubarizi – Kindai na Singidani,  Bicon ya Kati kati ya nchi , wanyapori na wengineo ndani ya kijiji na jiji la nyuki. Michezo na Burudani, na Kijiji cha nyuki Born -Fire

Previous articleSHAKA ATAKA HALMASHAURI KUWABANA WAKANDARASI
Next articleWIKI YA ASASI ZA KIRAIA (AZAKI) YAZINDULIWA RASMI JIJINI DAR
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here