Home LOCAL IDARA YA MAAFA YAWAPIGA MSASA WABUNGE.

IDARA YA MAAFA YAWAPIGA MSASA WABUNGE.

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Ummy Nderiananga akizungumza wakati wa Semina ya kuijengea uwezo Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria kuhusu Muswada wa Sheria ya Usimamizi wa Maafa iliyotolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu Agosti 31, 2022 Ukumbi wa Bunge, Jijini Dodoma.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Joseph Mhagama akifafanua jambo wakati semina hiyo.

Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Menejimenti ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Bwa. Charles Msangi akiwasilisha mada kuhusu Muswada wa Sheria ya Usimamizi wa Maafa mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria katika Ukumbi wa Bunge   Agosti 31, 2022 Jijini Dodoma.

Sehemu ya Wakuu wa Idara kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu wakifuatilia semina hiyo katika  Ukumbi wa Bunge  Agosti 31, 2022 Jijini Dodoma.

(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)

Idara ya Menenjimenti ya Maafa  imefanya semina ya kuwajengea uwezo wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria kuhusu Muswada wa Sheria ya Usimaizi wa Maafa ili kuwa na uelewa wa pamoja kuhusu sheria na namna zinavyofanya kazi pindi maafa yanapojitokeza.

Semina hiyo ilifanyika katika Ukumbi wa Bunge Jijini Dodoma ikihusisha wajumbe wote wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria iliyoandaliwa na Ofisi ya Waziri Mkuu.

Idara ya Menejimenti ya Maafa kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu imepewa jukumu la kuratibu na kushughulikia maafa na dharura zote ikijumuisha shughuli za Kuzuia, Kujiandaa, Kukabili na Kurejesha hali.

Viilevile Shughuli za kila siku za Idara zinaongozwa na Sera ya Taifa ya Usimamizi wa Maafa ya mwaka 2004 na sheria ya Menejimenti ya Maafa Na.7 ya mwaka 2015.

Previous articleWATOTO WOTE WAPEWE CHANJO YA POLIO, WAPOTOSHAJI TUTAWACHUKULIA HATUA: DC MBONEKO
Next articleKINANA ATUA KIGOMA KWA ZIARA YA KUIMARISHA CHAMA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here