Home Uncategorized HOSPITALI YA RUFAA YA KANDA CHATO MKOMBOZI KWA WANANCHI WA KANDA YA...

HOSPITALI YA RUFAA YA KANDA CHATO MKOMBOZI KWA WANANCHI WA KANDA YA ZIWA NA NCHI JIRANI HUDUMA ZA KIBIGWA.

 Muonekano wa mbele wa Hospitali ya Rufaa yw Kanda Chato Geita

Wakwanza kushoto ni Kaimu mkurugenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Chato wa pili ni Mkuu wa wilaya ya Chato mhe, Martha Mkupasi akifatiwa na Mkuu wa mkoa wa Geita Mhe, Martin Shigella.

Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhe, Martin Shigella akizungumza mara baada ya kukagua Hospitali ya Rufaa ya Kanda Chato
Mbunge wa jimbo la Chato Dkt. Medard Kalemani

Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhe, Martin Shigella akikagua moja ya kifaa cha kutolea huduma katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda Chato.

Kaimu Mkurugenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Chato wa nne kutoka Kulia akielezea jinsi wanavyotoa huduma mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhe, Martin Shigella wakwanza kutoka kulia

Kaimu Mkurugenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Chato Dkt. Brian Mawalla
Na: Costantine James, Geita.

Serikali ya Jamhuri ya muungano wa  Tanzania imetoa bilioni 9 kuendeleza ujenzi wa majengo mbalimbali katika hospitali ya Rufaa ya kanda chato kwa lengo la kuiwezesha hospitali hiyo kuweza kutoa huduma kwa wagojwa wengi zaidi hapa nchini.

Hayo yamebainishwa na Mkuu wa mkoa wa Geita Mhe, Martin Shigella katika ziara  yake wilayani chato akiambatana katibu tawala wa mkoa wa Geita Prof. Godius Kahyarara ziara ya kikazi pamoja na kujitambulisha kwa viongozi na watumishi wa wilaya ya chato.

Mhe, Shigella amesema seriali imetoa  fedha hizo kwa lengo la kueneleza ujenzi wa majengo pamoja na kuleta vifaa tiba katika haospitali hiyo ili kuweza kutoa huduma bora za matibabu kwa wananchi.

Amesema ukamilishwaji wa huduma mbalimbali za kibingwa katika hospitali ya Rufaa ya kanda chato utawezesha hospitali hiyo kutoa huduma bora zaidi kwa wananchi wanaozunguka mkoa wa Geita pamoja na mikoa jirani hapa nchini.

Amesema kukamilika kwa miundombinu pamoja na vifaa tiba katika hospitali hiyo wananchi wa mikoa ya kanda ya ziwa pamoja na nchi jirani kama vile kongo,Rwanda, Uganda kutawarahisishia zaidi kupata huduma za matibau hasa ya kibingwa kwani hawazuiliwi kuja kupata huduma katika hospitali hiyo.

Mkurungezi wa Hospitali ya Rufaa ya kanda chato Dkt. Brian Mawalla amesema hospitali hiyo ilianza kutoa huduma july 31, 2021 na mpaka kufikia july 30,2022 hospitali hiyo imehudumia wagojwa zaidi ya 10,500 kutoka mikoa ya kanda ya ziwa pamoja na nchi jirani

Dkt. Mawalla amesema hospitali hiyo inatoa huduma mbalimbali za kibingwa katika fani za Upasuaji,magojwa ya kina mama pamoja na kuwahudumia watoto, na sasa wanaendelea na kupanua wigo wa utoaji wa huduma kama vile kuanza kusafisha damu, ufunguzi wa jengo la ICU kwa ajiri ya wagonjwa mahututi.

Dkt. Mawalla amesema hospitali hiyo imekuwa msaada kwa wananchi kutoka  mikoa jirani ya kanda ya ziwa pamoja na kuhudumia wagojwa kutoka nje ya nchi katika magojwa ya upasuaji hivyo ujenzi wa hospitali hiyo chato umesogeza huduma za matibabu kwa wananchi.

Kwa upande wake Mbunge wa jimbo la Chato Dkt. Medard kalemani amesema kabla ya uwepo wa hospitali hiyo ya Rufaa ya kanda chato wananchi walikuwa wanapata shida kupata huduma za kibigwa na sasa wanapata huduma mbalimbali katika hospitali hiyo.

Dkt. Kalemani amempongeza mhe, Rais Samia Suluhu Hassani kwa kuwezesha kutoa pesa za ujenzi wa hospitali hiyo kwa awamu ya kwanza pamoja na kutoa pesa bilioni 9 kwa ajiri ya vifaa tiba ili kuwezesha kutoa huduma bora katika hospitali hiyo.

Nae Mkuu wa wilaya ya Chato Mhe, Martha Mkupasi ameishukuru serikali kwa kutoa zaidi ya bilioni 35 katika ujenzi wa hospitali hiyo na amemuhakikishia Mkuu wa mkoa wa Geita Mhe, Martin Shigella kusimamiavyema ujenzi wa majengo katika hospitali hiyi pamoja na kuhakikisha yanakamilika kwa wakati.

Mkupasi amesema wilaya ya chato itasimamia vyema matumizi ya fedha katika hospitali hiyo ili kuhakikisha fedha zinatumika kama ilivyokusudiwa pamoja na kusimamia majengo yanayojengwa yanajegwa kwa wakati  na kwa ubora unaohitajika.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here