Home LOCAL ‘HATUKURIDHIKA NA SHERIA ZA HABARI ZILIZOPITISHWA 2016’

‘HATUKURIDHIKA NA SHERIA ZA HABARI ZILIZOPITISHWA 2016’

WADAU wa habari tulianza kudai mabadiliko ya sheria za habari mapema, kwa kuwa sheria zilizopitishwa mwaka 2016 hatukuridhika nazo.

Kauli hiyo imetolewa na Neville Meena, Mjumbe wa Kamati Tendaji ya Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), wakati akizungumza katika Radio Mwangaza (Mwangaza FM), jijini Dodoma leo tarehe 17 Agosti 2022.

“Sheria ya Habari ya Mwaka 2016 ilipitishwa katika mazingira ambayo sisi wadau wa habari hatukuridhika, maeneo mengi ya msingi ambayo tuliyataka yawe sehemu ya sheria hiyo yaliachwa,” amesema Meena.

Meena amesema, baada ya sheria hiyo kupita wadau wa habari walikutana, na hapo ndio mchakato wa kutaka mabadiliko ya sheria hizo ulianza ingawa haukuwa na nguvu.

“Baada ya sheria hizi kupita na wadau kutokubaliana nazo, tulianza kudai mabadiliko lakini katika utawala uliopita hatukuona juhudi zozote zikifanywa na serikali.

“Utawala huu umeonesha toka mwanzo, ndio maana hata vyombo vya habari vilivyofungiwa Rais (Samia Suluhu Hassan) vilifunguliwa, tunaiona dhamira ya kweli,” amesema Meena.

Amesema, tayari mchakato huo upo katika mbalimbali na kwamba, ana matumaini makubwa ya mchakato huo kufikia malengo hata kama sio kwa asilimia 100.

“Tunayo matumaini ya kufikia malengo hata kama si kwa asilimia 100 tunayotaka, lakini mabadiliko bila shaka yatafanyika,” amesema.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here