Home LOCAL HABARI PICHA: KIKAO CHA WATAALAMU WABOBEZI WA MAGONJWA YASIYOPEWA KIPAUMBELE (NTDs)

HABARI PICHA: KIKAO CHA WATAALAMU WABOBEZI WA MAGONJWA YASIYOPEWA KIPAUMBELE (NTDs)

Picha mbalimbali za kikao cha wataalamu wabobezi katika Magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele (NTDs) yakiwemo Usubi, Matende na Mabusha, Trakoma, Kichocho na Minyoo kutoka nchini Tanzania na wadau kutoka USA, UK, WHO-HQ, WHO-Afro, WHO-TZ, KENYA na UGANDA

Lengo la kikao hicho ni kupitia kazi zilizofanyika Mwaka 2021/22 na mipango ya Wizara kupitia Mpango wa Taifa wa Magonjwa Yaliyokuwa Hayapewi Kipaumbele kwa Mwaka 2022/23 katika kutokomeza Magonjwa hayo (NTDs) na kushauri namna bora ya utekelezaji ili kufikia lengo la kutokomeza Magonjwa hayo ifikapo 2030.

Kikao hicho kinatekeleza agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. @samia_suluhu_hassan baada ya kusaini azimio la Kigali mnamo 27, Januari, 2022 lengo ikiwa ni kujitoa kwa 100% kuhakikisha Tanzania inatokomeza Magonjwa ya kitropiki yaliyokuwa hayapewi kipaumbele (NTDs) ifikapo 2030.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here