Home LOCAL DC ILALA AWAPONGEZA WENYEVITI WA MITAA, MABALOZI WA SHINA KWA KUTOA USHIRIKIANO...

DC ILALA AWAPONGEZA WENYEVITI WA MITAA, MABALOZI WA SHINA KWA KUTOA USHIRIKIANO ZOEZI LA SENSA

Na: Heri Shaaban (llala)

MKUU wa Wilaya ya Ilala Ng’wilabuzu Ndatwa Ludigija amewapongeza Wenyeviti wa Serikali za Mitaa Mabalozi wa Shina kwa kutoa ushirikiano katika zoezi la Kitaifa la sensa ya watu na Makazi Wilayani Ilala .

Mkuu wa Wilaya ya Ilala Ludigija alitoa pongezi hizo wakati wa kuzungumza na vyombo vya habari kuelezea mafanikio makubwa mpaka Sasa watu wamehesabiwa kwa asilimia kubwa na zoezi linaendelea mpaka Agosti 29/2022.

“Natoa pongezi kwa Wenyeviti wa Serikali za Mitaa ,Mabalozi wa Shina ,.Madiwani ,Watendaji ,makarani kwa kutoa ushirikiano katika zoezi la Kitaifa la sensa ya Watu na Makazi ndani ya Wilaya yangu ya Ilala “alisema Ludigija.

Aliwataka wenye kaya kuchukua orodha ya wapangaji wao na familia zilizolala siku ya Agosti 23/2022 kuwapatia makarani wa Sensa watakapofika katika nyumba yako.

Aliwaomba wananchi ambao hawajafikiwa na makarani wawe wavumilivu WOTE mwananchi hatahesabiwa, zoezi la sensa linafanyika kwa siku saba mpaka tarehe 29.08.22 hivyo wanapotoka waache taarifa za watu waliolala kwenye makazi yao tarehe 23.08.22 pamoja na namba za simu ili makarani wakifika iwe lahisi na kwa taarifa zitakazokosekana waweze kupigiwa simu waweze kuhesabiwa.

Alisema sensa ya Watu na Makazi kwa ajili ya maendeleo ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lazima ijue idadi ya Wananchi wake kwa ajili ya kupanga Mipango ya maendeleo ya Taifa.
Mwisho

Previous articleWIZARA ZAKUBALINA KUWEKA MIKAKATI THABITI KUBORESHA HUDUMA ZA MAKAZI YA WAZEE NCHINI
Next articleUANDISHI WA HABARI ZINAZOHUSU WATOTO UNAKABILIWA NA CHANGAMOTO KUBWA NCHINI
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here