Home BUSINESS BoT YAENDELEA KUTOA ELIMU KWA WANANCHI JIJINI MBEYA

BoT YAENDELEA KUTOA ELIMU KWA WANANCHI JIJINI MBEYA

Kaimu Meneja Idara ya Uhusiano wa Umma na Itifaki, Bi. Victoria Msina akimkabidhi Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Tulia Ackson, zawadi ya pochi ambazo pia hutumika kutoa elimu kwa wananchi kuhusu utunzaji sahihi wa noti.

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Tulia Ackson, akisalimiana na Mkurugenzi wa Tawi la BoT Mbeya, Bw. Ibrahim Malogoi, alipofika mapema leo katika banda la BoT kwenye Maonesho ya Nanenane yanayoendelea katika Viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya.


Mhasibu Mkuu Mwandamizi BoT, Bw. Elirehema Msemembo akitoa elimu kuhusu Alama za Usalama za Noti zetu kwa wananchi waliotembelea banda la BoT kwenye Maonesho ya Nanenane jijini Mbeya. Kulia kwake ni Meneja Msaidizi Idara ya Sarafu, Bw. Nixon Kyando.

Afisa Utawala Mwandamizi BoT, Bw. Dennis Alfred, akifafanua jambo kwa wananchi waliotembelea banda la BoT kwenye Maonesho ya Nanenane yanayoendelea katika Viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya.

Wachambuzi wa Masuala ya Fedha, Bw. Hassan Mbaga na Bi. Laila Kisombe wakitoa elimu kuhusu namna ya kuwekeza katika dhamana za serikali kwa wananchi waliotembelea banda la BoT kwenye Maonesho ya Nanenane yanayoendelea katika Viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya.

Afisa Mkuu Mwandamizi wa Benki, Bi. Joyce Njau, akielezea namna BoT inasimamia mifumo ya malipo nchini kwa wananchi waliotembelea banda la BoT kwenye Maonesho ya Nanenane yanayoendelea katika Viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya.
Previous articleMISA TAN YAKUSANYA MAONI NA MAPENDEKEZO YA WADAU KUBORESHA RASIMU YA UCHAMBUZI WA SHERIA ZA HABARI
Next articleWANANCHI WAMIMINIKA BANDA LA BRELA KUSAJILI BIASHARA ZAO MAONESHO YA NANENANE JIJINI MBEYA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here