Home LOCAL ‘BODI YA HABARI ISIMAMIWE NA WANAHABARI’

‘BODI YA HABARI ISIMAMIWE NA WANAHABARI’

SIO kweli kwamba waabdishi wa habari hawakosei wakati wakitekeleza majukumu yao, lakini tunasema makosa hayo ya kitaaluma yaendeshe kitaaluma.

Ni kauli ya Neville Meena, Mjumbe wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) na katibu mstaafu wa jukwaa hilo wakati akizungumza na Kituo cha Radio cha Nyemo, jijini Dodoma leo tarehe 17 Agosti 2022.

Amesema, mwandishi kama mwanataaluma yoyote, anaweza kukosea katika kazi yake lakini kumuwekea adhabu kubwa na yenye kuumiza, kunatishia uhai wa tasnia nzima ya habari.]
“Sio kweli kama mwandishi hafanyi makosa wakati anatekeleza majukumu yake, kama ilivyo kwa taaluma yoyote tunasema mwandishi atapofanya makosa ya kitaaluma basi ahukumiwe kitaaluma.

“Tumeona mwanasheria akifanya makosa anahukumiwa na bodi yao wenyewe, wahasibu wanahukumiana wenyewe kama ilivyo kwa madaktari; kwanini mwandishi asihukumiwe na Bodi ya Vyombo vya Habari inayoundwa na wanataaluma wanahabariu wenyewe? Badala yake serikali ndio inamuhukumu. Hii Hapana,’’ amesema Meena.

Pia Meena amesema, Sheria ya Vyombo vya Habari ya Mwaka 2016, ilikataliwa siku ya kwanza baada ya kusainiwa na kuanza kutumika kama mwongozo kwa vyombo vya habari nchini.
“Sheria ya Habari ya Mwaka 2016 ilipingwa na wadau wa habari siku moja baada ya kupitishwa ili kutumikaa. Si kwamba, hakukuwa na vitu muhimu kwa wanahabari, wadau waliona imebeba mitego na madhara mengi kwa wanahabari na vyombo vya habari,’’ amesema Meena.
Akizungumza kwenye Radio hiyo amesema, kutokana na yaliyomo kwenye sheria hiyo, wadau wa habari waliamini vyombo vya habari vitazidi kudumaa.

‘‘Tunashukuru hatua zilipofika kwa sasa. Rais (Ramia Suluhu Hassan) amekuwa na utashi wa kufanya mabadiliko lakini hata waziri aliyepo sasa (Nape Nnauye), mwelekeo wake ni huo,’’ amesema Meena.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here