Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) Adam Fimbo akionesha orodha ya Kemikali sumu zinazopatikana katika Bidhaa za Tumbaku alipokuwa akiongea na waandishi wa habari katika maonesho ya Kimataifa ya wadau wa bidhaa za afya ya Afrika Mashariki katika ukumbi wa Diamond Jubilee Jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Afrya Naibu Waziri wa Afya Dr.Godwin Mollel (wa pili kulia) akimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) Adam Fimbo (wa kwanza kulia aliyevaa suti) alipokuwa akizungumzia juu ya Kemikali sumu zinazopatikana katika Bidhaa za Tumbaku wakati waziri huyo alipotembelea katika banda la Mamlaka hiyo kwenye maonesho ya Kimataifa ya wadau wa bidhaa za afya ya Afrika Mashariki Jijini Dar es Salaam.
Meneja Mawasiliano na Elimu kwa Umma,wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (
(PICHA NA: HUGHES DUGILO)
 Na: Hughes Dugilo, DAR ES SALAAM
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) Bw. Adam Fimbo amesema kuwa Mamlaka hiyo imefanya uwekezaji katika mitambo ya kisasa inayoweza kubaini kemikali sumu zilizopo kwenye bidhaa za tumbaku kwa lengo la kulinda afya za wananchi wanaotumia bidhaa hizo.
Ameyasema hayo kwenye mahojiano maalumu yaliyofanyika kwenye Banda la Taasisi hiyo katika maonesho ya Kimataifa ya wadau wa bidhaa za afya ya Afrika Mashariki yaliyoanza leo agosti 30,2022Jijini Dar es Salaam ambapo amesema kuwa bidhaa za tumbaku zenye kemikali hizo zinaweza kusababisha magonjwa yasiyombukiza na kwamba TMDA imeweka orodha ya Kemikali zinazopatikana kwenye bidhaa hizo ikiwemo sigara kwa lengo la kutoa elimu kwa wananchi mbalimbali wanaotembelea maonesho hayo.
“kwa upande wetu sisi tunashiriki kwenye maonesho haya kwa lengo la kutoa elimu kwa wananchi wanaotembelea na hapa tumeleta orodha ya kemikali ambazo zipo kwenye bidhaa za tumbaku, Tunachokifanya sisi ni kupima bidhaa za tumbaku zikiwemo sigara ili kuhakikisha hizi kemikali haziwepo kwenye bidhaa hizo ”
“Hii ni horodha ya Kemikali sumu ambazo zipo kwenye Bidhaa za Tumbaku, horodha hii ya Kemikali ndizo zinazosababisha madhara kwa binadamu ukisikia magonjwa kama kansa ya koo, shinikizo la damu na magonjwa mengi yasiyoambukiza ambayo yanatokana na utumiaji wa tumbaku” Ameeleza Fimbo.
Ameongeza kuwa Mamlaka hiyo imefanya uwekezaji mkubwa kwenye mitambo kwaajili ya kupima na kubaini uwepo wa kemikali hizo kwenye bidhaa za tumbaku ili kuhakikisha kemikali hizo haziwepo kwenye bidhaa hizo.
“Tunataka hizi kemikali zisiwepo kwenye sigara kwa hiyo kazi yetu kubwa ni kuhakikisha kila sigara hazina hizi kemikali zilizopo hapa” ameongeza.Â