Home LOCAL DKT. MOLLEL: MSD WEKENI MPANGO WA MUDA MREFU KUPATA WAWEKEZAJI WA VIWANDA...

DKT. MOLLEL: MSD WEKENI MPANGO WA MUDA MREFU KUPATA WAWEKEZAJI WA VIWANDA VYA DAWA HAPA NCHINI

Naibu Waziri wa Afya Dr.Godwin Mollel (kulia) akizungumza na watumishi wa Bohari ya Dawa (MSD) alipotembelea Banda la Taasisi hiyo wakati wa uzinduzi wa maonesho ya Kimataifa ya wadau wa bidhaa za afya ya Afrika Mashariki yaliyoanza leo Agosti 30,2022 katika ukumbi wa Diamond Jubilee Jijini Dar es Salaam. (PICHA NA: HUGHES DUGILO)

DAR ES SALAAM.

Naibu Waziri wa Afya Dr.Godwin Mollel ameishauri Bohari ya Dawa (MSD) kutengeneza mpango wa muda mrefu wa kuzungumza na wawazalishaji dawa na bidhaa nyingine za afya kutoka nchi zinazozalisha bidhaa hizo kuja kuwekeza nchini Tanzania,hatua ambayo itarahisisha upatikanaji wa bidhaa za afya nchini.

Naibu waziri ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa maonesho ya Kimataifa ya wadau wa bidhaa za afya ya Afrika Mashariki yaliyoanza leo jijini Dar es Salaam.

Ameongeza kuwa MSD pia iangalie namna ya kuingia mikataba na nchi zinazozalisha bidhaa za afya kurahisisha kununua moja kwa moja kutoka kwao, ili kupunguza gharama na kuwezesha kupata bidhaa za kutosheleza mahitaji.

Kiongozi huyo pia amewahimiza wazalishaji hao wa nje kuja kuwekeza nchini Tanzania kwa kuingia ubia na serikali.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here