Home BUSINESS TRA YAWAFIKISHA MAHAKAMANI WATUHUMIWA SITA MOROGORO

TRA YAWAFIKISHA MAHAKAMANI WATUHUMIWA SITA MOROGORO

Na: Farida Mangube, Morogoro 
MAMLAKA ya mapato Tanzania TRA mkoa wa Morogoro, imewafikisha mahakamani watuhumiwa sita kwa makosa matatu likiwemo kuwazuia maafisa wa TRA kufanya kazi yao kwa kukataa kwa makusudi kurejesha fomu za VAT walizopewa, kinyume na kifungu cha 85 (3) (I) cha sheria  ya usimamuzi wa
Washitaki hao walifikishwa mahakama ya wilaya ya Kilosa tarehe 25 mwezi wa nane 2022 na kusomewa mashitaka  na  Mwendesha mashitaka  mwandamizi wa  Serikali Cherubini Chuwa mbele ya  hakimu mkazi mfawidhi   Agnes Ringo.
Washitakiwa  hao ni  Kibwana Kidinilo, Kitete Sugar, Clement Gwila  na Mathias Mligwa  ambao walifika mahakamani huku Gajoki LTD na Green Line Brothers hawakufika mahakamani hapo na hivyo mahakama iliagiza watafutwe na kufikisha mahakamani.
Akisoma mashitaka hayo mwendesha mashitaka Chuwa alisema washitakiwa hao walitenda kosa  hilo  Julai 26 mwaka huu, kwa nyakati tofauti wakati.
Alisema makosa wanayokabiliwa nayo ni kushindwa kuomba kusajiliwa kwenye kodi ya ongezeko la thamani VAT, kinyume kifungu  28 cha sheria ya kodi ya VAT sura 148, ikisomwa pamoja na kifungu Cha 90 (1) cha  sheria ya usimamuzi wa kodi  namba 10 ya mwaka 2015 yenye marejeo hadi mwaka 2019.
Alitaja kosa la pili ni kushindwa kuomba kusajiliwa kwenye kodi ya ongezeko la thamani VAT.
Alisema shitaka la tatu wanalokabiliwa nalo ni kushindwa kuendana na matakwa ya sheria za kodi kwa kutofika kwa hiari kusajiliwa na VAT.
Hata hivyo washitakiwa wote walikana mashitaka huku wakuachiwa kwa dhamana ya wathamini wawili wenye mali zisizohamishika zenye thamani ya sh milioni ishirini kila mmoja ambapo kesi hiyo itatajwa tena Agosi 31 mwaka huu.
Mwisho
Previous articleTANZANIA KUENDELEA KUDHIBITI MAGONJWA YALIYOKUWA HAYAPEWI KIPAUMBELE
Next articleRAIS. SAMIA APOKEA HATI ZA UTAMBULISHO KUTOKA KWA MABALOZI WANAOWAKILISHA NCHI ZAO TANZANIA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here